CHADEMA Wadai Mbowe Anakandamizwa



Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa CHADEMA Tumaini Makene, amesema kuwa licha ya kwamba Mwenyekiti wa chama hicho kushambuliwa na kuumizwa lakini bado ameendelea kukandamizwa kutokana na baadhi ya taarifa ambazo zinatolewa kuwa ni za makisio na si zile zinazotokana na uchunguzi.


Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe.

Makene ametoa kauli hiyo leo Juni 23, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, na kueleza hali ya Mbowe kuwa anaendelea vizuri, lakini wamekuwa wakishangazwa na matokeo ya uchunguzi uliotolewa, huku wakidai kuwa na mashaka kwani uchunguzi hauko huru wala wazi.

"Bahati mbaya kila ukisikia kauli za Polisi bado wanaonekana wameshatengeneza points za kumshambulia na kumkandamiza muathirika wa tukio la kuvamiwa na kushambuliwa, na wanakuwa wako 'very bias' tunakosa hata uchunguzi wa uhuru unaofanywa na Polisi badala ya kujielekeza kupata ukweli wa tukio ili mwisho wa siku kukomesha vitendo hivi" amesema Makene.

Mbowe alishambuliwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Juni 9, 2020, wakati akipandisha ngazi kuelekea nyumbani kwake Jijini Dodoma, ambapo baadaye taarifa ya Polisi ilitolewa na kuonesha kuwa siku ya tukio Mbowe alikuwa amelewa chakari.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mtadai Mnavyoona sawa wenyewe, Mtaingiaje Uraisi watu 11
    si mmeamua kumwekea Ribiti M/Kiti..!!

    Sasa Msigwa inakuwaje ili tujue tunafanyaje kumsaidia Mgonjwa wetu.

    ReplyDelete
  2. Mtadai Mnavyoona sawa wenyewe, Mtaingiaje Uraisi watu 11
    si mmeamua kumwekea Ribiti M/Kiti..!!

    Sasa Msigwa inakuwaje ili tujue tunafanyaje kumsaidia Mgonjwa wetu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad