CHADEMA Wataja Maendeleo Ya Freeman Mbowe




Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe anaendelea kupata uangalizi wa ziada chini ya Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Aga Khan, baada ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya ziada tangu alipofikishwa hospitalini hapo. 

 
Taarifa hiyo ya chama imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho Tumaini Makene na kusema kuwa uangalizi huo unahusisha saa 72 za kupumzika baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu wake wa kulia na uchunguzi wa ziada wa maeneo mengine ya mwili, uliofanyika siku ya Jumatano ambao bado unaendelea.

"Wakati tukiendelea kumtakia kila la heri Mwenyekiti Mbowe baada ya upasuaji huo ambao ni wa kwanza tangu aliposhambuliwa na kujeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili wake, pamoja na kwamba hatuna uhakika atalazimika kufanyiwa upasuaji mara ngapi au uchunguzi na matibabu ya ziada yatachukua muda gani na yatabaini nini, tunayo matumaini kuwa Mwenyezi Mungu atamsaidia kupona kwa haraka na kumrudisha katika siha njema" imeeleza taarifa hiyo.

Mbowe amekuwa katika Hospitali ya Aga Khan tangu Juni 9, 2020, alipofikishwa na kupokelewa kitengo cha dharura akitokea Dodoma baada ya kuvamiwa, kushambuliwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana alipokuwa akielekea nyumbani kwake. 

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Usanii Umemshinda ...Shalukani..


    Inachekesha... Faru John Kiboko..!!

    "tangu aliposhambuliwa na kujeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili wake, pamoja na kwamba hatuna uhakika atalazimika kufanyiwa upasuaji mara ngapi au uchunguzi na matibabu ya ziada yatachukua muda gani na yatabaini nini"


    Makene!

    Sasa kwa taarifa zaidi inahitajika

    Photoshop Editing kuongeza mazagazaga ili stetimentii ifanane.

    Halafu unamrudisha Jijini Dodoma aende kuendelea na mlolongo wa madai yake ikiwemo stetimenti crucial to Upelelezi.

    Kamanda Muroto anamsubiri . Tena haraka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huu ni Usanii wa next level...!!!

      Bebi... Una jibebisha mpaka unatetereka!!
      na Kuteguka... Hii mwanzo Mwisho...!!!

      Delete
  2. Silinde/Komu/Mollel/Ester/msgwa/Mwita/Lijualikali/Selazini/Lwakatare.

    Firimbi yenu ya Faulo tumeisikia na Tumeielewa , Asanteni sana. Usani unaendelea .. Enjoy the Show....!!

    Sacoozi ya Familia inaumbuka. Hizi ni baadhi ya akaunti ambazo zimekuwa akichotea Ruzuku na Posho

    NBC Account # 011103007155
    ECOBANK Account# 0020055401089601

    Zingine ziko Ughaibuni ambazo Mabeberu huwa wanamoatioa Huyu Kibaraka akishirikiana na wenzake katika Genge la Uvunjifu wa amani yetu na Usalama wake kiasi kwamba taifa letu lifikie hatima ya kuuzwa.

    Mbongo yuko kazini na Timu yake Mahiri. Huwa hawalazi zege

    Kwa upande wa Usani Muroto yupo!!

    ReplyDelete
  3. Huu ni Usanii wa Next Level...!!!

    Bebi... Una jibebisha mpaka unatetereka!! na Kuteguka...
    Hii mwanzo Mwisho...!!!


    " akitokea Dodoma baada ya kuvamiwa, kushambuliwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana alipokuwa akielekea nyumbani kwake".


    WASANII INAHITAJIKA YAFUATAYO:

    Photoshop Editing kuongeza mazagazaga ili stetimentii yako hapo juu ifanane.

    Halafu unamrudisha Jijini Dodoma aende kuendelea na mlolongo wa madai yake ikiwemo stetimenti crucial to Upelelezi.

    Kamanda Muroto anamsubiri .

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad