CHADEMA yapamba moto,Msigwa ataja mambo matatu




UCHUMI imara, kusimamia utawala bora na kuboresha elimu nchini, ndivyo vipaumbele vitatu ambavyo Mtia nia wa Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mch Peter Msigwa amevitaja. 

Mch Msigwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini ametangaza rasmi nia yake hiyo ya kugombea Urais kupitia Chadema leo jijini Dodoma ambapo pia alisindikizwa na wabunge wenzake, Godbless Lema, Joseph Mbilinyi 'Sugu' Hawa Mwaifunga na John Heche. 

Akizungumza na wandishi wa habari wakati wa kutangaza nia yake hiyo, Mch Msigwa amesema endapo atapata ridhaa ya kuwa Rais atahakikisha anafumua muundo mzima wa Elimu nchini na kuweka mwingine utakaokua na matokeo chanya kwa Taifa. 

Amesema mfumo wa elimu uliopo hivi sasa unaegemea zaidi vyeti na wala hauwapi wasomi mwanga wa kuwa wataalamu wa kuvumbua zaidi badala yake wanakua tegemezi ilihali ni wasomi. 



" Nikipata ridhaa ya kuwa Rais nitahakikisha nafanya maboresho makubwa kwenye elimu, ni lazima tuwe na Nchi ya wavumbuzi wanaotafuta suluhihisho kitaalamu, tuondokane na elimu ya vyeti ambayo kwa miaka 50 imeshindwa kuwakomboa watanzania. 

Kama Taifa hatuwezi kufanikiwa kwa kuwa na watu wenye fikra ndogo, tofauti yetu na wenzetu walioendelea ni upanuzi wa fikra na ukubwa wa elimu yao, tunapaswa kuwekeza kwenye elimu kama kweli tunataka kufikia uchumi wa kati unaotokana na viwanda, " Amesema Mch Msigwa. 

Akizungumzia ukuaji wa uchumi, Mch Msigwa amesema mfumo uliopo pia unahitaji mabadiliko makubwa kwani huu wa sasa umepitwa na wakati na hauwezi kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi. 

Amewaomba watanzania watakapoenda kuchagua Rais Oktoba 25 mwaka huu wachague Kiongozi mwenye maono ya kuwavusha kiuchumi na mwenye uwezo wa kuvutia wawekezaji na kutoa wigo mpana pia wa watanzania wenye kujiajiri. 

" Suala la utawala bora nitalisamamia kwa kuhakikisha pia tunarudish mchakato wa katiba mpya ambao utawezesha kubadilisha sheria kandamizi ambazo zimekua hazina msaada kwa watanzania zaidi ya kuwakandamiza. 

Kupitia mchakato wa katiba mpya naamini pia tutapata tume huru ya Uchaguzi ambayo itamaliza kiu ya watanzania lakini pia kuweka mgawanyo wa kimadaraka," Amesema Mch Msigwa. 

Mch Msigwa anakua mwanachama wa tatu wa Chadema kutangaza nia ya kugombea Urais hadharani baada ya wanachama wawili Mayjose Majinge na Makamu Mwenyekiti wa Chadema hiko, Tundu Lissu kutangaza azma yao ya kugombea kupitia chama hiko kikuu cha upinzani.

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Vichekesho ... Kibeko unataka nini.

    KIBEKO hata mchakato wa ndani ya Saccozi hutopita.

    Ila umejipa moyo kuwa siku katika maisha yako ulisimama na Bendera ya Taifa ikawa nyuma yako Ukatokea kwenye Online.

    Sasa Online presd alikuruhusu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivyo Kweli Uko Timamu au ndio vile?

      Delete
  2. Faru John... Anaendeleza machafuko Mitandaoni..... Uwiiiii!! tumeingiliwa..!!


    Faru John Kiboko..!!!!

    ReplyDelete
  3. Kibeko, Mie kura yangu Nakupa.
    Na kura ya Ubunge nampa Steve Nyerere!

    Dili hilo..

    ReplyDelete
  4. Mch Msigwa, Hongera mwanangu.

    unafaa kuliongoza hili genge.

    Naomba Baraza lako la Mawaziri.
    Ili nipate picha Kamili.

    Msigwa Oyee!! Steve Nyerere Oyee!!

    Mnagawana Ulaji. Poa! Tujulishe sherehe
    yako ya kuapizwa ili tujipange na nauli kukufata... KIBEKO oyeee!!

    Lakini Ngoja kwanza! Si wewe ulitujulisha kuwa Mzandiki na Muongo??

    au napoteza netiweki kama wewe?

    ReplyDelete
  5. Msigwa Kolona baba, Balakoa zinapatikana
    Bei poa.

    Mama Dkt MayRose amesha tangaza Nia Inatosha. Na kule online pia.
    Sasa amebaki Nyalandu na Wewe Nani Kuku nani Tai?

    Mie nakupa Kura ukinihakikishia kuwa Kiafya Uko Salama!

    Inatia wasiwasi Umetoka Karantini iku chache zilizopita. Tunaomba shahada kuwa uko free from Kolona!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nimemfatilia Nyalandu katika
      kutangazaNia kwake.

      Tukirudi kwa Kuku na Tai.

      Naona Nyalandu ni Tai. na wewe kama si Kibeko basi n Kifaranga.

      Delete
  6. (( KICHWA HUSIKA ))

    CHADEMA yapamba moto..!!!! INAPAMBAJE.??
    MTU KALALA MAJERUHI W FARU JONI NYUMBANI

    MBONA MNAHARIBU PROTOCOL.


    “Ripoti ya matibabu yake inaonesha ataendelea kupata matibabu na uangalizi wa karibu akiwa nyumbani hadi hali yake itakapoimarika kabisa na kupona,” amesema Makene


    ReplyDelete
  7. MCH MSIGWA. SASA UNATUCHANGANYA.

    KUHUSU KATIBA MPYA, MH. LIJUALIKALI ALISHA
    SEMA NA KUOMBA HATUWEZI KUITAKA KATIBA MPYA IKIWA YAKWETU HATUIFATI NA INATUSHINDA. HATA KUFIKIA NATURAL JUSTICE.. KWA TAARIFA YAKO CHAMA KILICHO FIKIA HATUA YA HOI BIN TAABAN .
    HATIMA YAKE NI KUFA AU IKIPONA BASI HUDHOHOFIKA SANA.. NDIO INAPOELEKEA.

    ReplyDelete
  8. MCH MSIGWA. SASA UNATUCHANGANYA.

    KUHUSU KATIBA MPYA, MH. LIJUALIKALI ALISHA SEMA NA KUOMBA HATUWEZI KUITAKA KATIBA MPYA IKIWA YAKWETU HATUIFATI NA INATUSHINDA. HATA KUFIKIA NATURAL JUSTICE.. KWA TAARIFA YAKO CHAMA KILICHO FIKIA HATUA YA HOI BIN TAABAN .
    HATIMA YAKE NI KUFA AU IKIPONA BASI HUDHOHOFIKA SANA.. NDIO INAPOELEKEA.

    ReplyDelete
  9. Hongera Mch Msigwa!!

    https://youtu.be/EpBDiKuNabY

    Kula yetu tunakupa!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad