Dar: Polisi lawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya dereva Uber, Mambosasa asimulia



JESHI la olisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya dereva tax(UBER) aliyefahamika kwa jina la Joseph Tillya Mpokala,(51),Mkazi wa Mbezi kwa Msuguli .



Akizungumza leo Juni 3,mwaka 2020, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amewataja watuhumiwa hao ni Godson Laurent Mzaura,(29),mkazi wa Mbezi Beach,Mpiga picha, Said Mohamed Mahadhi (38),Mkazi wa Afrikana,Fundi simu na Denis Urassa @ Pasua,(45),mkazi wa Makongo Juu,Fundi simu.

Kamanda Mambosasa amefafanua kuwa Mei 26, 2020 Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam lilipata taarifa kutoka kwa mke wa marehemu kuwa Mume wake ametoweka tangu tarehe 21.05.2020 na simu zake zote hazipatikani.

Amesema jeshi hilo kupitia kikosi chake cha kupambana na uhalifu kilianza ufuatiliaji mara mmoja na kwamba Mei 27, 2020 alikamatwa mtuhumiwa Godson Laurent Mzaura na kuhojiwa kisha kukiri kufanya mawasiliano na marehemu ambapo alieleza kuwa Mei 21,2020 saa saba mchana walimkodi marehemu ili awapeleke maeneo ya Mbezi.

“Na walipofika Mbezi Juu watuhumiwa hao walimuua Joseph Tillya na kumfukia kwenye shimo katika eneo la wazi lenye uzio wa ukuta ambao hujamalizika kujengwa(pagale). Juni 2, 2020 watuhumiwa wote watatu walihojiwa kwa kina na kukiri kuwa walifanya mauaji hayo na kuchukua gari la marehemu lenye T 139 DST Toyota IST na kwenda kulificha huko Kimara Baruti katika nyumba ya wageni ya Api Forest logde. “Jeshi la Polisi kanda Maalum Dar es Salaam linakamilsha taratibu za kupeleka jalada kwa mwasheria wa serikali na watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili,amesema Kamanda Mambosasa.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad