DC Kisarawe Awacharukia WATU Wazima Wanaowabaka Watoto



Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amekemea vikali sakata la vitendo vya utoro,mimba za utotoni pamoja na suala la  ubakaji kwa watoto wadogo vinavyofanywa na

baadhi ya watu wazima kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi kwani vinachangia kwa kiasi kikubwa kukatisha ndoto za watoto hao ambao wamezipanga  katika maisha

yao na kutaka   watu kama  hao wawajibishwe na chukuliwe hatua.

Kauli  ya Jokate ameitoa wakati wa ufunguzi rasmi wa  mkutano wa kikao  kazi kati ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ambao ulizijumuisha kata zote 17 ambazo ziliwakilishwa na Maofisa Tarafa, watendaji wa kata, watendaji wa vijiji pamoja na wenyeviti wa vijiji vipatavyo 84 kwa lengo la kujadili miradi mbali mbali  ya maendeleo na kuwataka wenyeviti na watendaji kuacha tabia ya kugombana na badala yake wajadili changamoto zinazowakabili.

“Kwa weli mkutano huu ni muhimu sana katika suala zima la kuleta maendeleo kwa wananchi wetu wa Wilaya ya Kisarawe, kwani tumeweza kuwakutanisha maofisa tarafa,watendaji wa kata, watendaji wa vijiji pamoja na wenyeviti mbali mbali wa vijiji,hivyo ninawaomba masuala mbali mbali yote ambayo tutayajadili hapa ni lazima tuyafanyie kazi hasa hii changamoto ya watoto wetu kufanyiwa vitendo vya ubakaji na watu wazima na wengine kujikuta wanakatisha masomo yao ni vema tukashirikiana kuanzia ngazi za chili ili kulitafutia ufumbuzi suala hili,”alisema Jokate.

Aidha Mkuu huyo alisema kwamba serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kuhakikisha inawaltea wananchi maendeleo ikiwemo kutoa elimu bora, hivyo hawezi kulifutia

mamcho sualo la watoto kutokana na vitendo wanavyofanyiwa na kuwataka wale wote ambao watabainika kuhusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe

fundisho kwa wengine wenye tabia kama hivyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama amesema kwamba lengo la kuwakutanisha viongozi na wawatendaji hao ni kufanya

tatmini ya utekelezaji wa majukumu ya kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo katika ngazi husika,ambapo pia ameahidi kuvalia njuga  maagizo yote ambayo yametolewa

na Mkuu wa Wilaya hasa suala la watoto wadogo kubakwa.

Gama alibainisha kuwa katika kikao kazi hicho kimeweza kuweka mipango mikakati kwa viongozi na watendaji katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo, ikiwemo

katika masuala ya kusimamia utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo sambamba na kufanya kazi kwa weledi na kuwatumikia wananchi wao kwa hali na mali lengo ikiwa

ni kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo,”alisema Gama.

 “Mimi kama mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe nimeamua kuwakutanisha viongozi mbali mbali wakiwemo maofisa tarafa, watendaji wa kata, watendaji

wa vijiji, pamoja na wenyeviti wa vijiji vipatavyo 84 ili kujadili changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu sambamba na kuwajengea uwezo katika suala zima la ukusanyaji wa mapato na utunzaji wa mazingira, afya, elimu na kujengewa uwezo sheria ambazo zinatumika katika majukumu yao ya kila siku,”alisema Gama.

Nao baadhi ya wenyeviti na watendaji ambao walihudhuria  katika kikao kazi hicho cha kazi akiwemo Mwenyekiti wa mji mdogo Ally Mkomwa na Mariamu Kimbeo mwenyekiti wa kijiji cha kikwete  wamekiri kuwepo kwa changamoto ya baadhi ya wanafunzi kukatisha masomo yao kutokana na kupata ujauzito pamoja na baadhi ya watu kuwabaka watoto  wadogo hali ambayo  wamedai inaruudisha nyuma  maendeleo ya sekta ya elimu hivyo jambo hilo watakwenda kulisimamia vilivyo ili kukomesha kabisa hali hiyo.

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe iliyopo katika Mkoa wa Pwani licha ya kupiga hatua za kimaendeleo katika baadhi ya sekta lakini bado imekuwa ikikabiliwa na  ngamoto ya watoto kukatisha masomo yao, wengine kupata mimba za utotoni, vitendo vya ubakaji kwa watoto wadogo ,hivyo kunahitajika juhudi za makusudi kutoka kwa serikali na wadau ili kukomesha hali hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad