Mama Dangote amekuwa motoni baada ya kulazimishwa na mashabiki wake kuomba Tanasha msamaha kwa kuita mwanawe kichwa kubwa.
Sasa dada yake Diamond Esma yuko motoni baada ya mashabiki kwenye mitandao ya kijamii kusema kuwa alihusika katika kutengana kwa Tanasha na Diamond.
Esma alisema kuwa amechoka kwa kusingiziwa kuwa alihusika na kusema kuwa watanzania ni wanafiki. Pia aliongeza na kusema kuwa hana wakati wa kuchunguza uhusiano wa kila mtu ilhali wake wazidi kuwa mbaya zaidi.
“Kwanza watu watambue kuwa mimi sihangaiki na uhusiano wa mtu kwa sababu ndoa yangu mwenyewe inawaka moto. Halafu wanafikiri wakiniita Yuda (Judas) nitabadilika kuwa Petro (Peter). Haiwezekani.” Alizungumza Esma.
Kwa wale hawafahamu uhusiano wa Esma na baby daddy wake umekuwa ukivunjika na kisha wanarudiana kila mara kwa mara tatu.
Kulingana na mwanabiashara huyo, afadhali aishi na wanawe wawili kwa maana wanaume hawajakuwa na uhusiano mwema naye.
Zari kwa muda hajakuwa na aibu kuwataja wanawake ambao ndugu yake Diamond amekuwa nao katika uhusiano wa kimapenzi.