Fatma Karume Arusha Kijembe Baada ya Kutenguliwa Viongozi wa Arusha



Wakili wa Kujitegemea, Fatma Karume achekelea taarifa ya kutumbuliwa kwa viongozi watatu wa Mkoa wa Arusha akiwemo Mkuu wa Mkoa huo, Mrisho Gambo.

Mbali na kicheko hicho Fatma alirusha kijembe katika ukurasa wake wa Twitter huku akiweka ujumbe huu ” Wakati wa uchaguzi matongotongo yanatoka machoni ubaya unaonekana,” aliandika ujumbe huo.


Rais John Magufuli amewatumbua viongozi watatu wa mkoa wa Arusha akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, imeeleza kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi wengine watakaoshika nyadhifa hizo.

Rais Magufuli amemteuwa  Idd Kimanta kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Kabla ya uteuzi huo  Kimanta alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha na kwamba nafasi hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli itajazwa baadaye.

Aidha, Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro na amemteua Kenan Kihongosi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Kabla ya uteuzi huo Kihongosi alikuwa  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Shangazi. Si uliwahi kuwa wakili zamani kabla ya kukushindwa kazi..!! Nasikia umeanzisha duka LA fesheni huko Ungonini.

    Hivi wewe wa Wapi?? Karibu nyumbani Tandahimba uone Babu na bibi WA babu. Kuna kolosho tu. Tena msimu huu zimezaa mpaka utapenda. Cameliusi alikuwa anakuongelea hivi punde. Tuna kumissi na koti jeusi kama zamani. Umeisikia Ofa ya DC

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad