Floyd Mayweather Amejitolea Kulipia Gharama zote za Mazishi ya Marehemu George Floyd


Floyd ametoa kiasi cha ($88,500) sawa na takribani milioni 204.7 za Kitanzania kulipia mazishi ya George ambaye aliuawa na askari wa kizungu wiki iliyopita.

Mayweather ame-share nasi hundi ya Kiasi hicho cha fedha ambacho amekiwasilisha kwenye familia ya marehemu. Mwakilishi wa Floyd Mayweather ameiambia TMZ kwamba familia ya George Floyd imekubali kupokea ofa hiyo.

Bondia huyo mstaafu ameguswa na kifo cha George sio tu kwa sababu ni Mmarekani mweusi, bali pia kutokana na CEO wa TMT Anzel Jennings kuwa mtu wake wa karibu na walipitia makuzi pamoja

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad