Habari Njema Kwa Mashabiki wa MPIRA Bongo...Mashabiki wa Soka Waruhusiwa Kuhudhuria Viwanjani...ila Kwa Masharti Haya



Serikali imesema katika ligi za soka na michezo mingine mashabiki waruhusiwe kuingia viwanjani kwa utaratibu wa kawaida. Mchezo utakaotathminiwa kuwa na mashabiki wengi, waruhusiwe kuingia na wasizidi nusu ya uwezo wa uwanja

Imeruhusu Ligi za soka ambazo Kanuni zinaruhusu kucheza nyumbani na ugenini kuendelea kuchezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini badala ya kutumia kituo kimoja ila mwongoza wa Afya uzingatiwe katika kusafiri, kukaa kambini na kwenye mazoezi

Aidha, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limetakiwa kuzingatia mwongozo wa Afya michezoni, liendelee kuratibu utekelezaji wa maelekezo ikiwemo kufanya tathmini na kutoa maelezo mahsusi juu ya namna ya kurejesha michezo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad