Hawa ndio viongozi wa CCM walichukua fomu ya kugombea Urais 2020 mpaka hivi sasa
0
June 18, 2020
Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM tayari viongozi mbalimbali wameanza kuchukua na kujaza fomu za kugombea Urais kwa tiketi ya chama hicho kwa mwaka 2020.
Leo mapema asubuhi Rais wa #Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, John Magufuli leo Juni 17, 2020 amechukua fomu za kuomba kuteuliwa na chama chake kuwania nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Mbali na JPM kuchukua fomu kupitia chama hicho pia Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi amechukua fomu za kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye nafasi ya urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao. lakini pia kwa upande huo wa Zanzibar Mbwana Yahaya Mwinyi, amekuwa mwanachama wa tatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujitokeza Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar, Kisiwandui, kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Omar Sheha Mussa, amekuwa mwanachama wa nne wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujitokeza Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar, Kisiwandui, kuchukuwa fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Amewahi kushika nafasi mbali mbali Serikalini ikiwemo Katibu Mkuu Wizara za Fedha na Afya katika Serikali ya awamu ya tano ya Zanzibar.
Mpaka hivi sasa hao ndio viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM ambao atayri wamechukua fomu ya kugombea Urais kwa mwaka 2020.
Tags