Hii Ndio Taa ya Ajabu Inayowaka TANGU Mwaka 1901 Mpaka Leo



Kuna maajabu mengi Duniani na mojawapo ni hili la Taa (Balbu), ambayo inashikilia rekodi ya kuwaka kwa muda mrefu zaidi.
Unaambiwa Balbu hiyo inawaka kuanzia mwaka 1901 na inapatikana huko Livermore, California Marekani na kitengo cha Zimamoto kutoka Livermore, ndiyo wamepewa mamlaka ya kuitunza na kuihudumia.

Kwa mwanzo Balbu hiyo inasemekana ilikuwa ikitoa nguvu ya mwanga yenye Watt 40 mpaka 60, lakini kwa sasa inatoa Watt 4 sababu ikitajwa ni kutokana na kukaa muda mrefu na mabadiliko ya teknolojia.

Balbu hiyo ilitengenezwa na kampuni ya Shebby Electric na inaelezwa kuwa taa nyingi zilizotengenezwa na kampuni hiyo miaka ya zamani mpaka sasa zinafanya kazi.

Zylpha Bernal Beck anasimulia kuwa Balbu hiyo ilitolewa na baba yake kwa kitengo hicho cha kupambana na moto mwaka 1901 ikiwa ni kama msaada.

Iligunduliwa mwaka 1972 na ripota aliyefahamika kwa jina la Mike Dustan, ambaye alifanya mahojiano na watu walioishi eneo hilo kwa muda mrefu na baadaye aliamua kuwaita watu wa 'Guinness Records' ambao walithibitisha kuwa Balbu hiyo imeweka rekodi ya kuwaka kwa muda mrefu zaidi.

Kwanini inawaka kwa muda mrefu?

Baadhi ya tafiti zilionesha kuwa kuwaka kwa Balbu hiyo kwa muda mrefu kunatokana na namna 'material' yake yalivyotengenezwa ambayo kwa kiasi kikubwa hulinda 'Vacuum' kwa lugha rahisi glassi yake isipoteze unga wake ambao ndiyo huwa chanzo kwa balbu nyingi kuzidiwa na kupasuka.

Balbu hiyo hutembelewa na watu wengi na kwa sasa kuna kitengo maalum kiliundwa, kwaajili ya kuhakikisha inabaki salama muda wote.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad