Bunge la Jmhuri ya Muungano wa Tanzania, limepitisha azimio la kumpongeza Rais John Magufuli kwa jinsi alivyoliongoza Taifa katika mapambano dhidi ya janga la virusi vya Corona.
Akiwasilisha azimio hilo, Mbunge wa viti maalum (CCM), Esther Mmasi katika kikao cha Arobaini na moja mkutano wa kumi na tisa wa bunge, Amesema mbinu na mikakati aliyofanya Rais imefanya nchi yetu kutoyumba kiuchumi na kuwezesha shughuli za maendelea kuendelea kama kawaida.
“Ameonesha uongozi thabiti ambao umewezesha kukabiliana na maambukiziya virusi vya Corona bila kuwatesa wananchi na bila kuathiri shughuli za kiuchumi za nchi yetu”. Amesema Mmasi
Aidha ametaja Mbinu na mikakati aliyotumia Rais zipatazo tisa ambazo wanaziunga mkono
Amesema Mosi, kuunda Kamati Maalum iliyoongozwa na Waziri Mkuu na Kikosi kazi cha kudhibiti na kukabiliana na janga la Corona; Mbili, kutenga hospitali na maeneo maalum ya kutoa huduma kwa watuwalioambukizwa virusi vya corona.
Tatu, kufunga kwa muda shule za awali, msingi na sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu; Nne, kusitisha shughuli zote za michezo, mikusanyiko, warsha na makongamano;
Tano, kuwaondoa hofu watanzania na badala yake kuwataka wauchukulie ugonjwa wa corona kama magonjwa mengine jambo ambalo kwa kiasi kikubwa lilipunguza hofu na taharuki iliyokuwepo katika jamii.
Sita, kukemea unyanyapaa (stigma) kwa wagonjwa wa Corona na miili ya watu waliopoteza maisha kwa ugonjwa wa corona. “Tulishuhudia Rais wetu akitoa tamko la kutaka wagonjwa wa corona wahudumiwe kama wagonjwa
wengine”
“Aidha, Rais wetu aliekeza mamlaka zake kuruhusu ndugu kuzika miili ya watu wao waliopoteza uhai kwa ugonjwa wa corona kwa kufuata mila na desturi zetu” Ameeleza Mmasi
Saba, kuruhusu shughuli za ibada kufanyika kwa kuzingatia maelekezo ya wataamu wa afya,Nane, kumtanguliza Mungu kwa kuwaomba viongozi wa dini na kuwahimiza watanzania kufunga na kumwomba Mwenyezi Mungu aliepushe taifa letu na
janga la ugonjwa wa corona.
Tisa, kuwataka watanzania kutumia mbinu mbadala kama vile kutumia dawa za asili ikiwemo kujifukiza.
“Mheshimiwa Spika, kutokana na mbinu na mikakati hiyo, taifa letu limeweza kuudhibiti ugonjwa wa corona ndio maana idadi ya wagonjwa na kasi ya kuenea kwa virusi vya corona imeshuka sana” Amesema Mbunge huyo.
Na kuongeza “Sasa hatuskii tena visa vipya vya wagonjwa wa corona wala vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa Corona.