Iran yaionya Marekani, kisa vikwazo vya silaha




Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa Majid Ravanchi amesema jana kuwa anaamini kwamba azimio la Marekani la kurefusha vikwazo vya silaha dhidi ya nchi yake hayatafanikiwa na kuonya kuwa itakuwa ”kosa kubwa” iwapo serikali ya Rais Donald Trump itajaribu kurejesha tena vikwazo vya Umoja wa Mataifa.

FILE - Iranian Ambassador to the United Nations Majid Takht Ravanchi speaks to the media outside Security Council chambers at the U.N. headquarters in New York, June 24, 2019. 

 

Ravanchi amesema kurejeshwa tena kwa vikwazo hivyo kutamaliza mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu na kuiondolea Iran majukumu yote katika makubaliano hayo.

Ravanchi amewaambia waandishi wa habari kuwa iwapo hilo litatokea, Iran haitakuwa chini ya kizuizi chochote kuhusu hatua itakazochukuwa na kwamba fursa zote zitakuwa wazi kwake.

Ravanchi amesema haya siku moja baada ya Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo kutishia kutafuta kurejeshwa kwa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran iwapo baraza la usalama la Umoja huo halitaidhinisha maazimio ya kuongeza kwa muda usiojulikana vikwazo hivyo vya silaha ambavyo muda wake ulikuwa unafikia mwisho mwezi Oktoba.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad