JE Wajua Mayai Yanaweza Kukusaidi Uishi Umri Mrefu? Soma Stori ya Huyu Mama Mwenye Miaka 117

Mwanamke aliyekuwa mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani (kabla hajafariki akiwa na umri wa miaka 117 na siku 137), aliwahi kutoa sababu iliyomuwezesha kuishi umri mkubwa kiasi hicho.

Emma Morano alikuwa ni raia wa Italia aliyezaliwa mwaka 1899, alipohojiwa na Shirika la Habari la Ufaransa (AFP) alipokuwa nyumbani kwake, alieleza alielezea chakula chake cha kila siku.

“Ninakula mayai mawili tu kila siku, basi,” Emma alinukuliwa akisema.

Lakini inawezekana siri haipo kwenye mayai anayokula, inawezekana siri kubwa imo katika jinsi ya anavyoyaandaa ― au kwa upande wake, kwa kutoyaandaa. Morano alisema kuwa amekuwa akila mayai mawili mabichi kila siku kwa miaka mingi sana tangu daktari wake alipomwambia kuwa yatamsaidia katika ugonjwa uliokuwa unaomsumbua wa upungufu wa damu.

Zaidi ya hilo, mwanamke huyu aliyekuwa na umri mkubwa zaidi alisema ameishi umri mkubwa na anashukuru kwa “kutotawaliwa”  na mtu yeyote na kwa kuishi peke yake tangu alipoachana na mumewe alipokuwa na umri wa miaka ya 30.

Daktari wake, Carlo Bava, anasema kwamba sio tu kuishi kwake kwa muda mrefu, bali hata afya yake na uimara alionao ni wa kushangaza.

“Mbali na magonjwa yanayompata lakini mara zote anarudi kwenye afya yake kama kawaida,” alisema kuliambia AFP. “Akisema yupo vizuri au anajisikia vizuri, ni kweli anakuwa vizuri kweli kweli.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad