Ni muda mrefu nimekuwa nafanya utafiti katika hii kanda ya mapenzi na kugundua kuwa wanaume wengi hufa kabla ya wake zao hata kama wamezaliwa mwaka mmoja na kubaini kuwa tabia za wake zao huwafadhaisha na kuwafanya waishi maisha magumu sana na kupata yale maradhi ya kufisha kama HYPERTENSION, SAIKOSISI, STROKE N.K
Pia kingine ambacho wazazi wa kike wanachokifanya ni kuwagombanisha watoto na baba yao uzeeni unakuta watoto wote hawako sawa na baba, unakuta wanamuhudumia mama tu pekeee, hata hela za matumizi anatumiwa mama ndo amgawie baba....baba anabaki mpweke na kujikuta anakufa haraka
Madhanio wakati wa utafiti ni kuwa je wanaume wasio katika ndoa je wanashambuliwa sana na magonjwa haya ya kufisha kama cohort wao walio katika ndoa? Hatimaye ikabainika kuwa wasio katika ndoa ni wachache sana karibu na hamna ila walio kwenye ndoa ni wote, kama sio aina moja ni nyingine. Hitimisho likawa wanawake huchangia vifo vya mapema vya wanaume katika ndoa.
Je, ni kwanini? Hii ni sehemu nyingine wazi ya utafiti.
Je. kuna aliyefanya utafiti binafsi kuhusu hili na nini hatima yake?
Nawasilisha!