Jeshi la Polisi Laanza Uchunguzi tukio la uvamizi alilofanyiwa Mbowe



JESHI la Polisi Mkoani Dodoma limethibitisha kushambuliwa na kujeruhiwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake jijini Dodoma.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema taarifa za Mbowe kushambuliwa na watu wasiojulikana walizipata asubuhi ya leo kupitia kwa Mbunge wa Viti Malum wa Chama hicho.

Muroto amesema tayari Jeshi la Polisi limeshaanza kufanya uchunguzi wa tukio hilo huku akiwaonya watu wanaosambaza taarifa za uongo pamoja na kupiga marufuku mikusanyiko yoyote isiyo halali.

" Tumepata taarifa za kuwepo kwa wanachama wa Chadema waliopanga kukusanyika kwenye ofisi za Chama cha hapa Dodoma, niwaonye kwamba Jeshi la Polisi halitoruhusu mikusanyiko kinyume na sheria na utaratibu.

Lakini pia tumelichukulia tukio hili kama tukio lingine la uhalifu na tayari tumeshaanza uchunguzi wetu, niwaonye wale wanaotaka kulitumia tukio hili kisiasa," Amesema Muroto.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad