Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo, amesema kuwa ile Tweet yake ya kwamba alipoteuliwa kwenye nafasi hiyo watu walimbeza na kumkejeli na kusema kuwa hilo halikuiwa dongo kwa mtu yeyote yule, bali alikuwa anajaribu kuelezea safari ya mwanadamu ilivyo fumbo kama kilivyo kifo.
DC Jokate ameyabainisha hayo Juni Mosi, 2020, wakati wa mazungumo maalum kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, na kusema kuwa maisha ya mwanadamu ni safari na hakuna anayeijua safari ya mwenzake na safari ikishaanza basi ni wachache sana ambao watakuunga mkono.
"Lile halikuwa dongo ilikuwa ni kuelezea safari ya mwanadamu, kwa sababu maisha ni fumbo, kama ilivyokuwa kifo, maisha ni safari na hakuna anayeijua safari ya mwenzake na kila hatua unayoipiga si kila mtu atakuunga wala kukutia moyo, unapoona hivyo si kwamba ufe moyo wewe songa mbele" amesema DC Jokate