JPM Apiga Marufuku Ujenzi wa Stendi Arusha Karibu na CCM “ya Watanzania Wote”



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa agizo kwa Mkurugenzi mpya wa Jiji la Arusha, Dkt. John Pima kuhakikisha stendi mpya ya kisasa iliyopangwa kujengwa Arusha inakamilika na haijengwi karibu na ofisi za CCM kwani ni ya watanzania wote.

Amebainisha hayo wakati akiwaapisha viongozi wapya leo, Juni 22, Ikulu jijini Dar es salaam na kuwapa tahadhari juu ya migogoro iliyoachwa na viongozi waliokuwepo awali mkoani Arusha.

“Palikuwa na mvutano mara stendi inajengwa huku, mara inajengwa huku, mara wanang’ang’ania ikajengwe kwenye ofisi ya CCM, ile stendi ni ya watanzania wote” Amesema Magufuli.

Ameongeza kuwa mvutano huo umewacheleweshea watu wa Arusha kupata stendi kama mikoa mingine na kusisitiza ni lazima ijengwe kwa kuepusha msongamano mjini ” Mimi ni mwana CCM lakini hatuwezi tukafanya mambo ambayo yapo nje ya utaratibu.

Aidha amebainisha kuwa ndani ya Serikali yake hataki migogoro na kwa yaliyotokea kwa viongozi wa Arusha yakawe fundisho kwa wengine kufuata viapo vya maadili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad