JPM Awapongeza Wasanii "Sio tu Zinaburudisha na Kuchangia Uchumi Wetu ila pia Zinaitangaza Nchi Kimataifa"



Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John P. Magufuli , ameitaja tasnia ya Sanaa na utamaduni Kama moja ya sekta iliyokua kwa kasi kubwa katika kuchangia pato la taifa tokea mwaka 2018.

Akizungumza katika hotuba ya kuhitimisha Bunge Jijini Dodoma , Raisi magufuli amesema kuwa kwa mwaka 2019 , Sekta hiyo ilishika nafasi ya 3 kwa ukuaji , huku akitaja Muziki wa Bongo Fleva kuwa moja ya sekta ya sanaa iliyochangia Pato la taifa kwa kiasi kikubwa.

Rais Magufuli amesema - "Kwa mujibu wa taarifa za hali Uchumi kwa mwaka 2018, shughuli za sanaa na burudani ziliongoza kwa ukuaji kwa mwaka 2018, ilikua kwa 13.7% . Mwaka 2019 ilishika nafasi ya 3 kwa ukuaji wa 11.2%. Hongereni Wasanii wetu wa Bongo Fleva, Filamu, na Michezo"
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad