Justine Bieber akana madai ya ubakaji anayodaiwa kufanya mwaka 2014



Mwanamuziki wa kimataifa wa miondoko aina ya R&B na Pop Justine Bieber amekanusha madai ya ubakaji yaliyojitokeza kwenye mtandao wa Twitter kupitia akaunti ya mtu asiyejulikana. 

Watu wawili wasiojulikana walituma ujumbe kwa njia ya Twitter wakidai kwamba unyanyasaji huo ulitokea mwaka 2014 na 2015. 

Akaunti ya mshtaki ambaye hajulikani imeondolewa kwenye mtandao wa Twitter lakini Justin Bieber amejibu na kusema: "Madai haya hayana ukweli wowote." 

Akaunti ya pili bado ipo kwenye mtandao huo wa Twitter. Akaunti hii mwenyewe anajulikana. 

Msemaji wa Justin Bieber amezungumza na Newsbeat ya BBC na kusema kwamba hakuna anachoweza kusema kuhusu madai hayo na kwamba hana cha kuongeza katika akaunti ya mtandao wa Twitter ya mwimbaji huyo. 

Justin Bieber alijibu madai hayo baada kuzungumza na mke wake na timu yake ambayo aliyakanusha vikali. 

Katika msururu wa ujumbe kwenye Twitter, mwimbaji huyo alituma picha kutoka kwa simu yake na ujumbe kuanzia usiku ambao unadaiwa madai hayo yalitokea 2014, ambao unaonesha mawasiliano yake na aliyekuwa mchumba wake Selena Gomez. 

Anasema kwamba wao hawakuwahi kuishi katika hoteli ya Four Seasons lakini alikuwa kwenye makazi ya kampuni ya AirBnB na marafiki zake. 

Pia, ametuma picha za ujumbe unaodai kwamba alionekana hoteli ya Four Seasons Machi 10, siku moja baada ya madai ambayo yanasemekana unyanyasaji huo ulitokea. Akaunti hiyo ya Twitter inaonekana kuwa imeondolewa. 

Newsbeat imezungumza na hoteli ya Four Seasons kutaka maoni yao. 

Justin Bieber pia ameoesha ujumbe kwenye barua yake pepe na risiti za kampuni ya AirBnB na hoteli ya Westin alikokuwa siku ambazo zimetiwa doa. 

Anasema alikuwa anatumia majina ambayo sio ya kweli ya Mike Lowery. 

Justin Bieber bado hajajibu shutuma za mtu wa pili ambaye anajulikana kwa jina la Kadi, anayedai kuwa alimnyanyasa katika hoteli ya New York Mei 2015. 

Newsbeat imezungumza na mwakilishi wake kutaka maoni yake kuhusiana na madai hayo ya pili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad