Kajala Amficha Bwana’ke Kisa Paula!




KAJALA Masanja ni mmoja wa mastaa ambao wana mvuto mkubwa sana ndani ya Bongo Muvi, mara nyingi anapenda kujiita Big Five yaani ni mmoja wa mastaa wenye nguvu kubwa kwenye tasnia.

Nguvu yao wanajinasibu ipo kuanzia jinsi walivyo, maisha wanayoishi na vitu vingine kibao.

Kwa kipindi kirefu, Kajala ameonekana kuwa tofauti kabisa na wasanii wengine, kwani amekuwa akipiga kazi zake na madili mbalimbali, na ni ngumu kumkuta kwenye kumbi mbalimbali za starehe kama ilivyokuwa huko nyuma.

Risasi Mchanganyiko limemtafuta mrembo huyo na kufunguka kama ifuatavyo:

Risasi: Habari za siku Kajala?

Kajala: Salama kabisa.

Risasi: Umekuwa kimya sana tofauti na huko nyuma, nini siri ya ukimya wako?

Kajala: Hakuna siri yoyote, ila tu nimeamua kufanya vitu vingine, pia achilia kazi ya uigizaji, lakini pia kuna maisha fulani nimeyaacha.

Risasi: Maisha gani hayo umeyaacha kwa faida ya wasomaji?

Kajala: Kuna maisha nilikuwa nayo nyuma, kutoka kwenda klabu na sehemu mbalimbali au kila kitu kikitokea nipo, ambacho kilikuwa si cha ulazima kabisa.

Risasi: Nini kimekufanya vyote uviweke pembeni?

Kajala: Ni mfumo wa maisha, unajua unaweza kuwa na hela nyingi ukashindwa jinsi ya kuzitumia au ukiwa hauna mpangilio, unazimaliza zote alafu baadaye unajuta kabisa.

Risasi: Unataka kutuambia misele uliyokuwa unapiga ilikuwa inakufilisi?

Kajala: Sana, yaani mtu unatoka mfukoni una milioni mbili, unarudi nyumbani una elfu 20.

Kwa kweli sasa hayo yalikuwa sio maisha. Niliamua kukaa na kutafakari kilicho bora maishani mwangu, nikaona ni bora kubadilika kwa sababu pia na umri nao unaenda.

Risasi: Wewe ni balozi wa Kampuni ya Biko, kampuni hiyo ina manafaa gani kwako?

Kajala: Kwa kweli maisha bila ya Biko yalikuwa ni magumu na ninamshukuru Mungu kanipa hiyo kazi imefanya niweze kuwa na nidhamu ya pesa kwa sababu ninaifanyia kazi kwa nguvu, naitumia kwa akili, maana unajua kama huna nidhamu ya fedha, hata ukiwa na ATM ndani, ni kazi bure tu.

Risasi: Umekuwa sio mtu wa kuwa na makundi au kuwa na rafiki mpaka kwenye mitandao, kwa nini?

Kajala: Sio kwamba sina watu wa karibu, lakini mambo ya mitandao siyapi nafasi sana kwenye maisha yangu, ndio maana napenda kuwa mimi kama mimi.

Risasi: Hali ni ngumu kwenye sanaa hata kwa wasanii, wewe ni Biko tu ndiyo inafanya uwe na maisha mazuri uliyonayo sasa hivi?

Kajala: Mimi pia ni balozi wa pedi ya Rania na kingine nidhamu tu ya matumizi ya fedha kama nilivyokwambia.

Risasi: Ukimuangalia Paula sasa hivi ni msichana mkubwa, nini unafanya kuhakikisha anakuwa na malezi bora?

Kajala: Kwa kweli napambana sana lakini kwa vile ni mtoto niliyemzaa, hanishindi hata kidogo, ananijua mama yake napenda nini na sitaki nini, heshima mbele siku zote.

Risasi: Ila naona na yeye sasa hivi anatumia mitandao ya kijamii maana ana akaunti yake, huoni kama ni hatari na yeye ni mwanafunzi?

Kajala: Hapana, yeye hana akaunti bali nafikiri kuna mtu kaifungua lakini sio yeye na mimi siwezi kukubali kwa sababu ni mama ninatambua mitandao inavyoharibu watoto.

Risasi: Kwa muda mrefu sasa hujawahi kumuweka mwanaume wako kwenye mitandao ya kijamii, ni kwamba hayupo au nini?

Kajala: Hapana, hata kama yupo, sidhani kama ni vyema watu wajue undani wa maisha yangu na isitoshe nina mtoto mkubwa sasa hivi.

Risasi: Mwili wako umeongezeka sana kwa sasa na huku unapiga mazoezi kila siku, au unapigilia msosi mno?

Kajala: Hapana kabisa, hivi sasa nimepungua sana, na ninafanya mazoezi.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad