Kaka wa George Floyd aitaka UN kuchukua hatua dhidi ya ubaguzi wa rangi




Nduguye marehemu George Floyd, Mmarekani mweusi aliyeuawa takriban wiki nne zilizopita, Philonise Floyd, amekiambia kikao maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi wa rangi, kuwa watu weusi nchini Marekani, wanataka usaidizi wa baraza hilo ili kulinda haki zao. 

Kwenye ujumbe wake aliouwasilisha kwa njia ya video, Philonise Floyd ameunga mkono pendekezo la nchi za Afrika kuutaka Umoja wa Mataifa kuanzisha uchunguzi rasmi kuhusu ukandamizaji wa haki, ubaguzi pamoja na ukatili wa polisi dhidi ya watu weusi nchini Marekani. 

Marehemu George Floyd alikufa Mei 25 baada ya polisi kuonekana akimkandamiza shingoni kwa goti kwa dakika kadhaa mjini Minneapolis. 

Nchi za Afrika zinataka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha pendekezo lao wiki hii na ibuni tume itakayochunguza mfumo wa kibaguzi na ukiukaji wa haki za Waafrika au za watu wenye asili ya Afrika.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad