IKIWA tayari siku mbili zimetimia tangu mtangazaji maarufu Hamisi Mandi ‘B Dozen’ kutangazwa rasmi kuwa amejiunga na E-FM & TV-E, Ijumaa hii amefunguka machache namna anavyokijua kituo hicho.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, B Dozen amekielezea kituo cha utangazaji cha E-FM (E-FM Company Limited) kuwa “Ni taasisi ambayo ina miaka sita tu kwenye game, lakini kasi yake inaonekana wazi’.
Ameongeza katika maelezo yake, “Naifahamu falsafa yao: falsafa ya muasisi Majizzo na taasisi yote. Naujua utamaduni wao, utamaduni wa kuthamini zaidi vya nyumbani hasa kuanzia kule mtaani chini kabisa. Nia yangu ya ndani inaniambia hapa ndipo ninapotaka kuwa kwa sasa.
My New Family Efm Tanzania na Tve Tanzania asanteni kwa kunikaribisha”. ameandika BDozen
Itakumbukwa, Dozen amekihama kituo cha CLOUDS FM ambacho amekifanyia kazi kwa takribani miaka 20, na kujiunga na kituo cha E-FM & TV-E.
Taarifa za B Dozen kuhamia E-FM zilitolewa kwa mara ya kwanza na Majizzo, ambaye ndiye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, kupitia ukurasa wake wa Instagram.