Kauli ya Basata Baada ya Kuruhusiwa Shughuli za Kisanaa Tanzania



Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), wametoa shukrani za dhati kwa Rais Magufuli kwa kurejesha shughuli za kisanaa kama ilivyokuwa awali, baada ya kuzuiliwa kwa muda kutokana na janga la Corona.


Akithibitisha hilo kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza amesema, walikuwa wamekaa vikao na wadau wote wa sanaa ili kujadili jinsi gani watafanya shughuli hizo licha ya uwepo wa ugonjwa wa Corona.

"Tayari tulikuwa tumekaa vikao na wadau wote wa sanaa siku ya Mei 28 ili kuangalia ni namna gani ambavyo tunaweza kufanya kazi zetu huku tunaishi na Corona, tulichukua yale maoni na tukapeleka Wizarani, ndiyo maana Rais mwenyewe alitoa tamko ili kurejesha shughuli za michezo, sanaa na burudani, na sisi kama BASATA tumetoa ruksa, lakini haina maana wasanii wavunje sheria na kanuni" Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad