Kituo cha Demokrasia na Teknolojia (CDT) kimewasilisha mashtaka dhidi ya amri ya Rais Donald Trump ya Kuzuia Udhibiti wa Maudhui Mtandaoni iliyosainiwa Mei 28, 2020
CDT inadai amri hiyo inakiuka Marekebisho ya Kwanza kwa kupunguza ubora wa taarifa za Taasisi na watu binafsi ziilizopo katika mitandao ya kijamii ambazo hulindwa Kikatiba
Kituo hicho kimesema amri hiyo imeundwa kuviondolea vyombo vya habari vya mitandaoni nguvu ya kuripoti na kupaza sauti kuhusu taarifa za upotoshaji, ukandamizaji wa wapiga kura, na ongezeko la vitendo vya uhalifu
Rais wa CDT, Alexandra Givens amesema upatikanaji wa taarifa sahihi kuhusu zoezi la upigaji kura na Uchaguzi Mkuu kwa ujumla ni nguzo ya demokrasia na Rais Trump ameonesha wazi kuwa lengo lake ni kutumia vitisho na kuvibana vyombo vya habari ili vibadili namna vinavyosimamia maudhui
Kituo hicho kimesema kimefungua mashtaka hayo kwasababu matendo ya Rais Trump ni ukiukwaji wa uhuru wa kujieleza na Serikali haitakiwa kulazimisha vyombo vya habari ya mtandaoni kusimamia maudhui kwa kuangalia kile ambacho Rais anataka