Korea Kaskazini Kuongeza idadi ya Askari wake Karibu na eneo la Mpaka wa Korea mbili
0
June 18, 2020
Korea Kaskazini inapanga kurejesha mazoezi ya kijeshi kwenye mpaka wake na Korea Kusini na kuwapeleka wanajeshi katika maeneo ambayo awali yalikuwa vituo vya pamoja ya viwanda na utalii, wakati mzozo kuhusu kampeni ya wanaharakati wa Korea Kusini ya kusambaza vipeperushi ukipamba moto.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali, uongozi wa jeshi la Korea Kaskazini umesema wanajeshi watatumwa katika eneo la kiviwanda katika mji wa mpakani wa Kaesong pamoja na Milima ya Kumgang katika pwani ya mashariki.
Vituo vya ulinzi katika eneo la kijeshi kati ya nchi hizo mbili vitafunguliwa tena na kampeni ya kulipiza ya usambazaji vipeperusi dhidi ya Korea Kusini itaanzishwa.
Mipango hiyo ya Pyongyang inafanyika siku moja baada ya kuiripua na kuiharibu ofisi ya mawasiliano kati ya Korea mbili katika upande wake wa mpaka mjini Kaesong.
Tags