Naamini mapenzi hayalazimishwi wala hayashikiwii Mtutu.
Pia naamini kwa dhati kabisa penzi linapokwisha ni bora watu watengane tu. Hakuna ndoa kama upendo haupo au maelewano hayapo.
Ndoa ni maelewano na makubaliano ya watu walio oana kimtazamo,kiuchumi, kidini na mambo Kede Kede. Haya yanapokosekana hakuna ndoa na usilazimishe upendo..
Kuna upuuzi fulani wa kumfumania mtu na kumlawiti mwanaume mwenzako au kumuua kabisa
Mimi naamini wanawake ni watu timamu na wenye maamuzi sahihi kabisa. Ukiona mke wako amekusaliti, achana naye.
Ukristo unaruhusu ndoa kuvunjika sababu ya uzinzi lakini pia hairuhusu kisasi kwa namna yoyote ile wala hauruhusu kuua mtu sababu ya usaliti.
Mara nyingi wanawake hutoka na kutafuta wanaume wenyewe. Lakini hata akitafutwa ana haki ya kukataa. Kuna wakati wanawake wengine huvua hata pete za ndoa mavyuoni humu na hata maeneo mengine
Kulazimisha mapenzi ni ujinga wa kiwango chake. Mpe mwanamke mziki aupendao uone kama atatoka kama umeoa mke kweli.
Kulikuwa na mwanamke fulani anakwenda kusema kwa mume wake kila akitongozwa. Siku kasema katongozwa na fulani na mume anamfahamu kaenda speed kwa jamaa. Kufika kule ugomvi ukaanza. Jamaa mwenye mke kapigwa na kupata ulemavu mpaka leo. Nani kasababisha haya?. Mke bila shaka.
Nimalizie kwa kusema huwezi kummiliki mtu. Mtu ana moyo wake na maamuzi yake. Mtendee wema mkeo na kama yuko kamili hatokusaliti. Lakini kama ulioa yule wa mwanaume mashine usiingie hatiani kuua au kulawiti mwanaume mwenzako sababu ya maamuzi ya mtu aliye timamu kabisa.
Mabaya mawili hayaleti usahihi.