Kutolewa Saudia katika orodha ya fedheha ya kuua watoto, ni fedheha




Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameulaumu vikali Umoja wa Mataifa kwa misimamo yake ya kindumilakuwili katika kadhia ya haki za binadamu na kusema, kitendo cha umoja huo cha kuitoa Saudi Arabia kwenye orodha nyeusi ya wavunjaji wa haki za watoto ni fedheha, kinaudhi na kimewakasirisha wengi. 

Sayyid Abbas Mousavi amesema hayo usiku wa kuamkia leo Jumatano wakati akijibu hatua ya Umoja wa Mataifa ya kuliondoa jina la muungano wa Saudi Arabia katika orodha ya wavunjaji wa haki za watoto na sambamba na kuelezea kusikitishwa kwake na jambo hilo amesema, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameuondoa muungano wa Saudia unaofanya mauaji makubwa ya raia wasio na ulinzi wa Yemen katika orodha hiyo wakati ambapo mashirika ya kimataifa yamekiri kuwa muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia umefanya jinai kubwa dhidi ya watoto wa Yemen kama vile kushambulia basi lilikuwa na wanafunzi, mashambulio katika makazi ya raia, maskuli na mahospitali na kuua idadi kubwa ya watoto na kuna ushahidi wa wazi kabisa wa picha na video za kutisha za kudhitibisha jinai hizo. 



Vile vile amesema, kisingizio kilichotumiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa cha kuutoa muungano vamizi wa Saudia katika orodha ya fedheha ya kuua watoto wadogo nchini Yemen kinashtua na kinaudhi vibaya. Itakukmbukwa kuwa Antonio Guterres ametoa matamshi ya kejeli kwa kusema, "ni watoto 222 tu" ndio waliouawa na kupata madhara katika mashambulio ya muungano wa Saudi Arabia nchini Yemen. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, kwa kitendo chake hicho na kwa matamshi yake hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonesha kuwa kuuliwa na kupata madhara watoto 222 wa Yemen si jambo muhimu kwake. 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad