Aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, amesema kukosekana uelewa wameshusha thamani ya Tanzanite kwa hali ya juu.
“Piece ya kilo 9.27 na 5.28 ni unique pieces ambazo kwa bei mnayo pigia kelele sio zaidi ya USD 3.5 milioni,” aliandika Lema katika ukurasa wake wa twitter.
“Najiuliza sasa ni pieces gani nyingine zitapata thamani kuonyesha upekee wa madini haya,” aliandika Lema.
Lema amesema madini hayo ambayo ni adimu bei zake hazipangwi kwa gramu isipokuwa upekee.
“Kuna rules katika biashara hizi, rules hizo hazihitaji degree/PHD isipokuwa wall street thinking. Nani ataona thamani ya Tanzanite kwa kilo 9.27/5.28 kuuzwa sawa na saa ya Mike Tyson na mnunuzi ni serikali?,” aliandika Lema.
Kwa kukosa uelewa mmeshusha thamani ya Tanzanite kwa hali ya juu sana, piece ya kilo 9.27 na 5.28 ni unique pieces ambazo kwa bei mnayo pigia kelele sio zaidi ya USD 3.5 milioni.Najiuliza sasa ni pieces gani nyingine zitapata thamani kuonyesha upekee wa madini haya ?— Godbless E.J. Lema (@godbless_lema) June 25, 2020
Uliekuwa mbunge, INAKUHUSU..??
ReplyDeleteUmeshakuwa dealer..?? Nyammaza angalia
ajira mpya hapo stendi. ya Mtori au
Gereji itapendeza. Ya Sigara kubwa
Utaingia matatani.
Godilesi, tumesha kusahau.
ReplyDeleteSiuliwahi kuwa mbunge kipindi kilicho
pita?
Sasa uko wapi mwenzetu? na chama gani?