Mwanamuziki Lil Wayne Atoa Mtazamo WAKE wa Maandamano Yanayoendelea Marekani "Nilisaidiwa na Askari wa Kizungu"

Lil Wayne anatofautiana kimtazamo na wengi kwenye sakata hili la kutetea haki za mtu mweusi ambalo linaendelea kwa maandamano nchini Marekani na dunia kufuatia kifo cha George Floyd.

Kwenye mahojiano na Fat Joe wiki kadhaa zilizopita, Wayne alisema tusilichukulie kwa ujumla tukio hili na kuwashushia lawama idara yote ya polisi, bali tuangalie matendo ya askari mmoja mmoja kwani sio wote ni wabaya, kauli ambayo haikupokelewa vyema na jamii ya watu weusi.

Ijumaa ya wiki iliyomalizika, Wayne ameibuka tena na kuitetea hoja yake kwa kusema kwenye maisha yake aliwahi kusaidiwa na askari wa kizungu
-
"Maisha yangu yaliokolewa na askari wa kizungu nilipokuwa na umri mdogo. Nilikuwa na miaka 12 hivi, Nilijipiga risasi mwenyewe, na niliokolewa na askari wa kizungu, anaitwa Robert Hoobler au Uncle Bob. Hivyo inapaswa kuelewa namna ninavyo watazama polisi. Nilisaidiwa na askari mzungu." alisema Lil Wayne na kukazia
-
"Walikuwepo baadhi ya askari weusi ambao waliruka na kukimbia waliponiona nimejipiga risasi kifuani. Walichokuwa wakisema ni tumeona silaha na vitu vingine, lakini Uncle Bob nilimsikia akisema nimemkuta huyu mtoto kalala sakafuni, nahitaji kumpeleka hospitali wala hakusubiri ambulance, alitumia gari yake." alimaliza Wayne kwenye mazungumzo kupitia Young Money Radio.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad