Liverpool Kumbe Walikuwa Mabingwa EPL Tangu Mechi ya Nane


“KUMBE ndivyo ilivyo?, baada ya mechi nane, hongera kwa Liverpool kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England,” alinukuliwa kocha wa Manchester City, Pep Guardiola akiipongeza Liverpool licha ya kuchezwa michezo nane tu.

Inaweza kufikirisha, bingwa wa Ligi Kuu England aliwahi kupatikana mapema? Tuangalie historia ilivyokuwa japo dalili zinaonyesha Liverpool wamefanya vizuri.

Wakati huu ambao ligi inatarajiwa kurudi baada ya mapumziko huku timu zingine zikicheza michezo yao ya kirafiki au kikosi kimoja kujigawa mara mbili.

Mara baada ya Guardiola kuitabiriwa ubingwa Liverpool huku michezo nane ikiwa imechezwa, je, misimu mingine ya nyuma ilikuaje baada ya idadi hiyo ya mechi?

2018/19

Unakumbuka jinsi Maurizio Sarri alivyouanza msimu huo bila kufungwa akiwa na timu yake ya Chelsea? Kilikuwa kipindi ambacho walicheza mpira mzuri na kusumbua wapinzani huku akimtambulisha kiungo Jorginho ndani ya Ligi Kuu England.

Kama ilivyotarajiwa, Manchester City na Liverpool walikabana koo tangu mwanzo wa Ligi Kuu mpaka mwishoni, huku Arsenal na Tottenham walianza msimu vizuri lakini wote walionekana hoi mwishoni mwa ligi.

Bournemouth walikuwa moto wa kuotea mbali, walikuwa moja ya timu sita za juu baada ya michezo nane huku Manchester United ikiwa nafasi ya 13, yaani pointi nne mbele ya klabu zilizopigania kushuka daraja.

2017/18

Ulikuwa msimu ulioanza kwa kasi, itakumbukwa Ronald Koeman wa Everton na Jose Mourinho aliyekuwa Manchester United walikuwa vizuri.

Naye, Marco Silva na kikosi chake cha Watford walikuwa katika mbio hizo ndani ya mechi nane za kwanza kabla hajatimuliwa Januari. Walicheza mpira mzuri dhidi ya Liverpool na Arsenal.

Vijana wa Jurgen Klopp walicheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huo, waliuanza msimu taratibu kwa kushinda mara tatu, sare nne na kufungwa mmmoja na kuwaacha nafasi ya nane.

2016/17

Kama watu walidhani msimu huu ungeisha baada ya mechi nane tu, basi Manchester City wangepewa kombe lao hata kabla ya msimu kuanza.

Wakali Leicester City ambao walitwaa ubingwa msimu mmoja nyuma, hawakuwa vizuri katika msimu huo mpya baada ya michezo nane ya kwanza.

Manchester City walipata kichapo kutoka kwa Tottenham, huku Arsenal wakimaliza nje ya timu nne za juu kwa mara ya kwanza chini ya Arsene Wenger licha ya kuanza msimu vizuri.

Mabingwa walikuwa Chelsea ambao walitumia mfumo wa 3-4-3 chini ya Antonio Conte kushinda michezo yao, upande mwingine, Manchester United haikuwa vizuri, japo Mourinho aliwapa matumaini makubwa.

2015/16

Si rahisi kuusimulia. Ulikuwa mmoja wa msimu mgumu ndani ya historia ya Ligi Kuu England, labda mpaka sasa hakukuwa na msimu kama huo.

Manuel Pellegrini aliitengeneza Manchester City ambayo ilikuwa huru kufunga mabao, alifanikiwa kunasa saini za Raheem Sterling na Kevin de Bruyne. Arsenal na Manchester United walikuwa nyuma, huku Leicester City wakisubiri kuandika historia.

Tottenham ambao walikuwa katika mbio za ubingwa walikuwa nafasi ya nane wakiwa na pointi 13 huku Chelsea wakiwa wa 16 na pointi zao nane, moja pungufu kwa Manchester United sasa.

2014/15

Chelsea walionyesha dalili za kuwa mabingwa tangu kwenye maandalizi ya msimu wa 2014/15. Ilikuwa timu iliyofanya vizuri chini ya Jose Mourinho aliyerejea kutoka Real Madrid.

Manchester City hawakuwa vizuri, walishindwa kukimbizana na Chelsea kwenye mbio za ubingwa licha ya kumsajili Frank Lampard.

Baada ya kushinda michezo mitano kati ya nane, Chelsea walikuwa kileleni huku Southampton na West Ham zikiingia kwenye orodha ya timu sita za juu. Ulikuwa msimu mbaya kwa Liverpool na Manchester United ambao waliuanza vibaya.

2013/14

Unakumbuka nini kuhusu msimu huu? Basi iko hivi, Arsenal walifanikiwa kunasa saini ya Mesut Ozil aliyekuwa akicheza Real Madrid. Vijana hao wa Wenger waliuanza vizuri msimu na kuwa moja ya timu zilizokuwa katika mbio za ubingwa baada ya mechi nane.

Msimu wa kwanza wa Mourinho aliingia Chelsea akitokea Real Madrid, hakuwa na msimu mzuri huku Manchester City wakiwa tayari wamepachika mabao 20 baada ya mechi nane.

Naye, David Moyes alikuwa kocha wa Manchester United akirithi mikoba ya Sir Alex Ferguson, walikuwa na pointi 11 baada ya michezo nane.

2012/13

Nadhani kila mmoja anamkumbuka Roberto Di Matteo wa Chelsea ambaye aliiongoza klabu hiyo kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu mmoja nyuma yake akiwa kama kocha wa muda.

Sir Alex Ferguson ulikuwa msimu wa mwisho kwake na kikosi cha Manchester United ambao alitwaa ubingwa huo kwa kuwasajili akina Robin van Persie, Shinji Kagawa, Nick Powel na wengine.

Manchester City walikuwa nafasi ya pili, Arsenal waliuanza msimu taratibu lakini walimaliza vizuri kwa kuwa ndani ya timu nne za juu
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad