Kocha wa Yanga Luc Eymael amewashushia lawama Viongozi wa klabu yake kwa kushindwa kumkatia tiketi kutoka Ubelgiji ili arejee Tanzania ambapo kwenye Interview na goal.com amesema “Viongozi wa Yanga wananiambia wameshindwa kunikatia tiketi ya ndege kwenye system, kama wameshindwa kunikatia katika system basi wangenikatia online”
“Ni vizuri kusaini mkataba na LaLiga lakini kama unataka kuwa klabu kubwa kwanza jaribu kumrudisha kocha wako haraka iwezekanavyo kama una muheshimu”