Maandamano Kutokana na Kifo cha George Floyd Yaendelea Katika Miji Mbalimbali Nchini Marekani
0
June 01, 2020
Waandamanaji wanaopinga ubaguzi kwa mara nyingine tena wameingia mitaani katika miji nchini Marekani jana Jumapili kupaza sauti zao za hasira dhidi ya ukatili wa polisi.
Wakati huo huo utawala wa rais Donald Trump uliwaita wanaoongoza maandamano hayo yaliyofanyika katika usiku wa siku tano kuwa ni magaidi wa ndani.
Rais Trump aliwapongeza wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa taifa kwa kusema, "pongezi kwa walinzi wetu wa taifa kwa kazi nzuri waliyofanya mara walipowasili Minneapolis , Minesota, usiku wa jana," alisema hayo katika ukurasa wa Twitter
Waandamanaji walichoma moto karibu na Ikulu ya Marekani ya White House wakati hali ya wasi wasi na polisi ilipopanda wakati wa siku ya tatu mfululizo ya maandamano ya usiku yaliyofanyika kujibu kifo cha George Floyd mikononi mwa polisi mjini huko Minesota.
Waandamanaji pia walikusanya vibao vya alama za barabarani na vizuwizi vya plastiki na kuchoma moto katikakti ya mtaa H. ..Baadhi walishusha bendera ya marekani kutoka katika jengo la karibu na kuitupa katika moto
Tags