Makete:Binti Atoroka Nyumbani kwa Tuhuma za Kusababisha Kusambaa kwa Video ya Mtoto ikihusishwa na Ushirikina
0
June 28, 2020
Familia ya Bw.Mussa Sanga mkazi wa kijiji na kata ya Bulongwa wilaya ya Makete mkoani Njombe imeiomba jamii na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuto isambaza video ya mtoto wao inayohusishwa na imani za ushirikina na kutakiwa kupuuza kwani haina mahusiano kabisa na vitendo hivyo
Katika video hiyo ameonekana mtoto wa kiume aliyekaa ndani ya ungo na chini yakiwa yameanikwa mahindi akijibizana na dada yake
'‘Tunapandaga ndege amesema mtoto,na nani aliulizwa,na Bibi tunaenda kwa mama mkubwa mama Samwel,mnaenda mnakaba! Eeeh ,Mnapanda Humu? Eeh’' baadhi ya majibizano ya mtoto na binti
Kufuatia video hiyo kusambaa huku ikimhusisha mtoto huyo na imani za kishirikina hasa baada ya kukaa kwenye ungo wazazi wa mtoto huyo, Mussa Sanga na Getruda Ntale wameitaka jamii kutomhusisha mtoto au familia yao na imani za kishirikina,kwani binti aliyerekodi na kuweka status (WHATSAPP) video hiyo na kusababisha kupakuliwa hakuwa na maana hiyo na kwamba walikuwa wanacheza kwani dada huyo aitwaye Amina Ebron Msitu ni mpenzi wa watoto na kwa sasa amekimbia nyumbani baada ya video hiyo kuendelea kusambaa mitandaoni.
‘'Yeye amesema walikuwa wanafanya utani,sasa alianzaje kuweka mtandaoni hata kama anasema tumsamehee,tunamsame vipi ingali video hii imesambaa nchi nzima! arudi amsafishe mtoto na bibi yake!"alisema mama wa mtoto
‘'Mimi ninachohitaji aje tu ajirekodi video kumsafisha mtoto wangu na kukanusha,mama yangu mimi sio mchawi hata jamii inayotuzunguka inajua hilo,hilo tu ninalohitaji kwa sasa’' alisema Mussa Sanga baba wa mtoto.
Baba wa binti aliyerekodi video hiyo Mch.Ebron Msitu amesema ni kweli binti yake alifanya hivyo lakini wanaomba watanzania kuipuuza video hiyo na kuacha kuisambaza kwani ni udhalilishaji wa mtoto mdogo huku akimtaka binti yake popote alipo kurejea nyumbani ili kukiri kosa kuliko alivyokimbia.
‘'Tunaendelea kumtafuta maana tangu aondoke mawasiliano hayapo tena,amefunga simu zote,Na tulipompigia simu alisema kweli baba mimi tulikuwa tunacheza na mtoto (mdogo wangu) wala hizo tafsili zinazotafsiliwa sio kweli,mimi ni mpenzi wa watoto napenda kucheza na watoto’' alisema Mch.Ebron Msitu
Familia ya Bw.Mussa kwa sasa imesema ipo katika wakati mgumu sana hasa baada ya tukio hilo la kusambaa kwa video ya mtoto wao.
Tags