Makonda Atoa Shavu kwa Wasanii wa Dar es salaam..." Basata Wafungulieni Wafanye Matamasha"


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka wanaotangaza kuwa Dar sio sehemu salama waache mara moja kufanya hivyo huku akiwaomba Baraza la Sanaa la Tanzania (BASATA), kuruhusu wasanii wa Dar es salaam kufanya matamasha.


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda

Makanda ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na viongozi wa dini, ambapo amesisitiza mambo mbalimbali ikiwemo kutoa onyo kwa watu wanaoichafua Dar es salaa.

''Nashindwa kuelewa nia ya watu wanaosema Hospitali zimefurika wagonjwa wa Corona wakati nchi yetu Mungu ameikoa na tunaendelea na maisha na sasa nchi mbalimbali zimeanza kutuiga sisi, naomba sana watu wanaofanya hivyo waache'', amesema.

Aidha Makonda amesema hali sasa imeshakuwa shwari na pengine Baraza la Sanaa nchini sasa liangalie uwezekano wa kuwaruhusu wasanii wa Dar es salaam waanze kufanya matamasha ili wajipatie kipato
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad