Makosa Ambayo Watoto wa Zamani Walikuwa Wakila Bakora.....


*MAKOSA AMBAYO WATOTO WA ZAMANI WALIKUWA WAKILA BAKORA!!*
*WATOTO WA ZAMANI TULIISHI MAJUMBANI KAMA TUKO MAFUNZO YA JESHI!! UKIKUA NI FULL ADABU KUHESHIMU WATU, UTU, BUSARA NA KUJITETEGEMEA UKIWA NA UMRI MDOGO TU:*
1: Usiposalimia wakubwa asubuhi unapigwa
2: Usiposalimia wageni unapigwa
3: Ukinawa kabla ya wageni unapigwa
4: Ukilia bila sababu unapigwa
5: Ukinyanyuka wakati wa kula kabla ya wakubwa kuinuka unapigwa
6: Wakubwa wakiwa wamekaa wewe ukaenda kusimana pembeni unapigwa
7: Ukikaa wakubwa wamesimama unapigwa
8: Ukitumwa dukani ukachelewa kurudi unapigwa
9: Ukichelewa kurudi toka shuleni unapigwa
10. Ukiwahi kurudi shuleni unapigwa
11: Ukililia wageni wakati wanaondoka , wakitoka unapigwa
12: Kujipitisha pitisha wageni wakiwa wanakula unapigwa
13: Kujibu ovyo wakubwa unapigwa
14: Kutukana watu wazima, watoto au rika lako unapigwa
15: Ukiwa mbishi bila sababu unapigwa
16:Ukipigwa ukalia unapigwa ili unyamaze
17: Ukipigwa umenyamaza unapigwa ili ulie
18: Ukipigwa shuleni ukaenda kusema nyumbani, unapigwa
19: Ukianza kula nyama kabla ya wakubwa unapigwa
20: Ukila kwa jirani ukabainika unapigwa
21: Ukianza kunawisha wenyeji badala ya wageni mkimaliza kula unaitwa chumbani unapigwa
22: Ukianza kunawisha watoto badala ya wakubwa unapigwa
23. Ukimkuta mtu nzima hujampokea unapigwa
24. Ukienda kusema kama umepigwa unapigwa.
25. Mtu mzima akipita kama mnacheza hamjamshughulikia unapigwa.
26. Ukienda nyumba za watu, ukaona kitu au ukasikia story ukaileta nyumbani unapigwa
27. Ukipewa hela na mtu asiefahamika au hata anaejulikana inategemea mazingira gani unapigwa
28. Ukianza kuchaguwa chakula hiki nakula hiki sili unapigwa
29. Ukianza kuwa na marafiki wasioleweka makwao unapigwa
30. Mtu mkubwa akija kukuchongea nyumbani hata kama sio cha ukweli unapigwa
31 ukimwambia mtu mzima muongo unapigwa
32 ukila ukimtazama mtu uson unapigwa
33 ukila ule mbele yako ukizid kwa mwenzako unapigwa
34 magharib uwe ushaingia ndani ukichelewa unapigwa
35 tv kikimaliza kipindi cha watoto tu ukitizama cha watu wazima unapigwa
36 ukimaliza kula km hujaondowa vyombo na kuvikosha unapigwa
I like this😄👆
Nyongeza:
37. Kukojowa kitandani unapigwa
38. Ukipigana unapigwa
39. Ukasema uongo unapigwa.
40. Ukipoteza pesa unapigwa!

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Swadakta, Ndivyo tulivyo Kuleeeni.
    Na Leo tunafuraha na Kujivunia kuwaona
    kwamba mmekuwa Wakurugenzi, na Ma-CEO.
    Na Mnajituma na Heshma na Adabu kwetu
    na kWa Walimwengu. ni KIZAZI CHENYE
    MAADILI na TAMADUNI nzuri Tulizorithi
    toka kwa Babu Zenu.

    Mwangalie DC Chalamila,Dkt Bashiru Ali, Hamis Kigwangalla, M.Gambo, S.Jafo, Robert Kabudi, Palamagamba Kabudi, J. Ndugai, S.H Suluhu, A.H Mwinyi, K, Majaliwa. H.Zungu, Shivji.
    J.Magufuli, J. Malecela, P.Msekwa.
    A.Sapi (Mrh) J.Lusinde, P.Bomani, J.Kijazi, Mabeyo, S.Iboni, A.Diwani,
    Mkuchika, Kichere. Hao ni baadhi tu
    ambao ukiwaangali utajua kwamba Malezi Bora na Mila na Desturi Zimewaingia katika DNA zao inavyo stahiki.

    Wana Utu,Uungwana,Ustaarabu na Heshma.
    Kwa hiyo haina shaka wataleta vizazi
    bora.

    Tumekuleeni inayo paswa na kustahiki.
    Mungu akubarikini kuendelea kutujali
    na zamu yenu hii kutulea sisi..

    Tuliwapiga kwa Faida ambayo sasa mmeiona na kuongoka.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad