Maisha yako ili yazidi kuimarika kila wakati yanahitaji kuwa na mtiririko ambao unaeleweka kila wakati. Kama hakutakuwa na mtiririko ambao unaeleweka huwa ni sawa na kuvaa kiatu kwanza kisha uvae soksi, hii ina maana hauna mtiririko ambao unaeleweka, na kufanya hivyo kuandaa makao ya kufa maskini.
Hivyo katika maisha yako ili uweze kuona mabadiliko kila wakati unahitaji kuwa na mambo makubwa mawili ambayo yatakusaidia kufika mbali zaidi. Na mambo hayo ni lazima uweze kuyafanyia kazi kwa ufasaha na ufanisi wa kutosha. Na mambo hayo ni;-
1. DIRA.
Dira ni alama ambayo husaidia kuonesha uelekeo hii ni kwa mujibu wa mwalimu wangu wa somo la maarifa ya jamii. Ambapo mwalimu wangu alisema dira hii husaidia kuonesha pande nne za dunia ambazo ni mashariki, kusini, magharibi na kaskazini.
Baada ya kutufundisha hivyo niligundua ya kwamba kumbe dira ni ya muhimu sana kwani inatusaidia kujua uelekeo ni wapi ambapo tunaelekea, na nikawaza kumbe bila ya kuwepo kwa dira watu wengi tungekuwa tunapotea sana.
Kwa kutumia mfano kifaa hicho hicho cha DIRA kinachotusaidia kujua ni wapi ambapo tunaelekea, nimegundua kifaa hiki ni lazima kila mwanadamu aweze kukiweka katika fikra zake ili kimuoneshe ni wapi ambapo anaelekea katika kupata mafanikio ya maisha yako na jamii kwa ujumla.
Wengi wetu hatuna kifaa hiki katika fikra zetu, wengi hatujui ni wapi ambapo tunaenda, pia wengi hatujui tunataka nini katika maisha yetu. Kutukujua ni nini ambacho tunakitaka na wapi ambapo tunaekekea huko ndiko kutojua thamani ya "dira".
Wengi wetu tumekata tamaa kabisa, na ndio maana tukiulizana mwenzangu unataka kufanya nini kwa sasa? Ambacho kitakutoa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine wengi husema mimi nitafanya chochote, bila shaka kwa muktadha huo utagundua ya kwamba bila shaka hutujuai ni kitu gani ambacho tunakitaka, kwa maneno mengine tunaweza kusema hutuna DIRA.
Najaribu kuwaza kwa sauti ni kwa nini hatuna dira ambayo itasaidia kufika mbali zaidi? Nichokuja kugundua ni kwamba hatuna dira ya maisha kwa kuwa hatujui tunataka nini katika maidha yetu.
Hivyo ni wakati mwafaka kwako kuweza kujitengenezea kifaa hicho katika fikra zako kwa kujua ni nini ambacho unataka? baada ya kujua nini ambacho unakitaka unachotakiwa kufanya ni kuwaza je! unawezaje kufika huko ambako unataka kwenda? Baada ya kupata majibu anza kuweka mipango mikakati ambayo itakufanya uweze kufika huko ambako unataka.
2. KANUNI.
Baada ya kuona jambo la kwanza ambalo ni muhimu kulifahamu, jambo la pili ambalo ni muhimu kulifahamu ni kwamba unatakiwa kuwa na kanuni za mafanikio, kanuni ndiyo msingi wa kufikia dira. Bila kujua kanuni na misingi kufikia dira ya mafanikio itakuwa ni ngumu.
Hivyo kanuni ndiyo njia sahihi ya kupata jawabu la changamoto fulani, hivyo kama kuna changamoto ni lazima uweze kutafuta kanuni ambazo zitakusaidia kuweza kutatua changamoto.
Kwa maneno mengine tunaweza tukasema ya kwamba kanuni ndio msingi wa maisha yako, na dira ndio ukuta wa mafaniko yako.