Rais wa Marekani Donald Trump amesema alikunywa dawa ya hydroxychloroquine kwa wiki mbili
Matumizi ya dharura ya dawa ya kutibu ugonjwa wa malaria ya hydroxychloroquine kama tib aya virusi vya corona yamefutwa kulingana na Shirika la Usimamizi wa Chakula na Dawa la Marekani (FDA).
Shirika la (FDA) limesema kwamba ushahidi mpya kutoka kwa taasisi za afya umeonesha kuwa hakuna haja ya kuendelea kutumia dawa hiyo kwa matumaini kwamba inaweza kukabiliana na ugonjwa wa virusi.
Rais Donald Trump alitetea matumizi ya dawa hiyo ya hydroxychloroquine kama tiba ya ugonjwa wa Covid-19.
Machi, Shirika la FDA lilitoa idhini ya matumizi ya dawa hiyo kwa wagonjwa ambao watakuwa wanaumwa sana.
Lakini Jumatatu, shirika hilo lilisema kwamba utafiti wa kwenye taasisi ulipendekeza kwamba dawa ya hydroxychloroquine haina ufanisi kwa kutibu ugonjwa huo wa virusi na kushindwa kuzuia maambukizi miongoni mwa waliopata maambukizi.
Akijibu uamuzi uliochukuliwa na Shirika la Usimamizi wa Chakula na Dawa la Marekani (FDA), Trump alisema yeye amekuwa dawa hiyo kama kinga na hakupata madhara yoyote.
"Niliinywa na nikahisi vizuri," aliwaambia wanahabari Jumatatu, na kuongeza: "Sina malalmishi kuhusu dawa hiyo, niliinywa kwa wiki mbili, na niko hapa, tuko hapa sote."
Rais huyo, 74, alisema kwamba watu wengi walimwambia kwamba dawa hiyo imenusuru maisha yao.
Mei, Bwana Trump aliweka wazi kwamba anakunywa dawa hiyo ya kutibu ugonjwa wa malaria baada ya watu wengine katika Ikulu kuthibishwa kwamba wameambukizwavirusi vya corona.
Maoni yake kuhusu dawa ya hydroxychloroquine ulikuwa gumzo liilosambaa katika mitandao ya kijamii na kuleta utata ndani ya tasnia ya wanasayansi kuhusu manufaa na athari za dawa hiyo pamoja na dawa nyingine yenye uhusiano wa karibu ya chloroquine.
Majaribio ya matumizi ya dawa hiyo yalisitishwa kote duniani pale jarida la Lancet lilipochapisha utafiti wake unaoonesha kuwa dawa hiyo imeongeza idadi ya vifo na matatizo ya moyo kwa baadhi ya wagonjwa.
Matokeo hayo yalifanya Shirika la Afya Dunia (WHO) na mengine kusitisha majaribio kwasababu za kiusalama.
Hata hivyo, jarida la Lancet pia nalo liliondoa utafiti huo baada ya kubainika kwamba ulikuwa na mapungufu mengi na WHO imeanzisha tena majaribio ya