Matokeo ya awali Malawi yaashiria ushindi wa upinzani



Matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais uliorudiwa nchini Malawi yanaonyesha kuwa mgombea wa upinzani Lazarus Chakwera anaongoza kwa asilimia 60, dhidi ya mgombea wa chama tawala ambaye pia ni rais wa sasa Peter Mutharika. 

Hayo ni kulingana na ujumuishaji wa kura ambao umefanywa na kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali MBC. Kulingana na takwimu za kituo hicho,, Rais Peter Mutharika amepata asilimia 39 ya kura. 

Mapema siku ya Alhamisi, chama cha upinzani kilimtangaza mgombea wao Lazarus Chakwera mshindi, lakini tume inayosimamia uchaguzi imewaambia waandishi wa habari kwamba itawachukua siku mbili au tatu zaidi hadi kupata matokeo rasmi. 

Kambi ya Rais Mutharika bado haijatoa tamko lolote kuhusu matokeo hayo ya awali. 


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad