Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare Arudi CUF Kutumika Kuiangamiza Chadema

Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare amehamia Chama cha Wananchi (CUF) na kupokelewa na Maftah Nachuma, Makamu Mwenyekiti wa CUF Bara katika Ofisi Kuu za chama hicho zilizopo Buguruni, Dar
-
Lwakatare, alitangaza kustaafu siasa Aprili 14, 2020 akiwa Bungeni na kusema hana mpango wa kugombea Ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 na kuwa hatojiunga na chama chochote cha siasa
-
Akitoa sababu za kwenda kinyume na msimamo wake wa kustaafu siasa, amesema CUF ilimuomba arudi na yeye ni miongoni mwa watu waliokiasisi chama cha hicho, hivyo amerudi ili kuhakikisha chama hicho kinaimarika
-
Lwakatare alivuliwa uanachama CHADEMA, kwa kosa la kukaidi agizo la kutohudhuria vikao vya Bunge kama tahadhari dhidi ya ugonjwa wa #COVID19
-
Akizungumzia kuhusu hatma ya Ubunge wake, Lwakatare amesema yeye ni Mbunge anayetambuliwa na Ofisi ya Spika wa Bunge baada ya chama chake kumfukuza
-
Aidha, CUF imesema itamtumia Mbunge huyo kuvimaliza vyama vya upinzani hususan CHADEMA, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MH LWAKATARE KWENDA CUF...!!

    What A Choice...!!!!

    Saccozi ya Mtowe inaangamia kutoka katika Ulingo wa Siasa Malumbano of their Choice.

    Lwakatare alikuwa ni Miongoni mwa Nguzo za Siasa Bora katika Sakozi.

    Akili zake timamu na ukataaji wa Kupelekeshwa ndizo hisia zilizompelekea
    kujinasua kimawazo kutoka Gengeni kwa Wapotoshaji. Hongera sana Mh Lwakatare.

    ReplyDelete
  2. MH LWAKATARE KWENDA CUF...!!

  3. MH LWAKATARE KWENDA CUF...!!

Top Post Ad

Below Post Ad