Mchezaji Molinga Aijia Juu Yanga



WAKATI kukiwa na taraifa kuwa nyota wa Yanga, Mkongoman , David Molinga amegoma kusafiri na kikosi hicho mkoani Shinyanga, straika huyo amewajia juu waajiri wake hao na kudai anashangazwa kuona kila jambo baya lazima hausishwe.

Yanga iliondoka alfajiri ya jana kwenda Shinyanga ambako Jumamosi inakabiliwa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Kambarage.

Kabla ya safari ya Shinyanga, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli alitoa orodha ya wachezaji 22 watakaosafiri akiwemo Molinga, lakini baadae ilibainika waondoka ni 19, huku watatu wakisalia Dar es Salama akiwemo Mkongomani huyo.

Taarifa kutoka Yanga ilidai Molinga aligoma kuambatana na wenzake, huku ikielezwa kuwa alimwambia Meneja wa timu, Abeid Mziba, kuwa haoni sababu ya kocha kumjumuisha Benard Morrison na Haruna Niyonzima, kwakua hawakufanya mazoezi ya kitimu kama watasafiri yeye hatokwenda.

Lakini Molinga alikanusha jambo hilo huku akisema amekuja Tanzania kucheza mpira na tangu timu ilipoanza mazoezi ameshiriki kikamilifu na kushangazwa taarifa ya yeye kugoma kwenda Shinyanga.

“Jana listi ilitoka na mimi jina langu alikuwepo sasa inasemekana vipi mimi nimegoma kama ndio hivyo muulizeni kocha ndio alitajia listi yake, nachukizwa kusikia mara kwa mara kila kitu mimi tu hata kama sijafanya kitu kibaya utasikia tu Molinga ‘this is too much.”

Molinga aliongeza: “Molinga atapita Yanga itabaki, hakuna haja ya kuchafuliana majina, tusubiri miezi miwili iishe ili tumalizane, kila mtu atapita tu Yanga.”

Katika kikosi cha Yanga , Molinga ndiye kinara wa mabao msimu huu akiwa amefunga mara tisa, nane kwenye ligi na moja kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC).

Kikosi cha wachezaji 19 wa Yanga kilichoondoka kwenda Shinyanga jana kinaundwa na kipa Farouk Shikhalo, Metacha Mnata, mabeki Paul Godfrey, Juma Abdul, Adeyum Saleh, Jaffary Mohamed, Kelvin Yondani, Lamine Moro na Saidi Makapu.

Wengine ni viungo Abdulaziz Makame, Feisal Salum Abdallah, Mapinduzi Balama, Haruna Niyonzima, Mrisho Ngassa, Deus Kaseke na Patrick Sibomana.

Washambuliji ni Yikpe Gnamien, Ditram Nchimbi na Tariq Seif.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad