Msajili Avionya Vyama Vinavyopanga Kushirikiana Uchaguzi Mkuu



Mvutano juu ya Mikutano ya Siasa: Msajili Msaidizi wa Vyama vya ...Msajili msaidizi wa vyama vya siasa nchini Sisty Nyahoza amevionya vyama vya siasa vilivyopanga kushirikiana kwenye uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mapema mwezi oktoba kwa kudai kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria ya vyama vya siasa kifungu cha 11 (a)

Akizungumza mjini Dodoma msajili amesema mpaka sasa ofisi yake haijapokea maombi yoyote au makubaliano ya vyama husika juu ya kushirikiana kwao na muda wa kuwasilisha maelezo hayo umepita kisheria hivyo vyama vitakavyofanya hivyo vitakuwa vinavunja sheria

“Vyama havijakatazwa kushirikiana bali vimewekewa utaratibu ili Tume ya Uchaguzi pamoja na taasisi zote zinazohusika na uchaguzi ziweze kujiandaa vizuri na kuimarisha ulinzi hasa wakati wa kampeni pamoja na kuvisaidia vyama vingine kuelewa wanashindana na vyama vya aina gani,” amesema Nyahoza.

Ikumbukwe kuwa baadhi ya vyama vya upinzani nchini  vimetangaza kufungua milango ya kushirikiana na vyama vingine kwa lengo la kuweka nguvu pamoja ili kuking’oa chama cha CCM madarakani
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad