Mshukiwa wa Mauaji ya Watalaamu wa UN nchini Congo Akamatwa


Mmoja wa washukiwa wakuu katika mauaji ya watalaamu wa Umoja wa Mataifa waliokuwa wakichunguza makaburi ya halaiki katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekamatwa baada ya msako wa miaka mitatu ya kiongozi huyo wa kundi la wapiganaji.

 Mkuu wa ofisi ya mwendesha mashitaka wa jeshi katika eneo hilo ameliambia shirika la habari la AFP kuwa Tresor Mputu Kankonde alikamatwa Jumamosi na anapelelezwa kwa sasa.

Luteni Kanali Jean-Blaise Bwamulundu Kuzola amesema Kankonde anatuhumiwa kwa makosa kadhaa yakiwemo mauaji ya watalaamu wa Umoja wa Mataifa.

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa Zaida Catalan na Michael Sharp, mwanamke wa Sweden mwenye asili ya Chile na mwanaume wa Kimarekani, waliuawa mnamo Machi 2017 katika mkoa wa Kasai ya Kati.

Walikuwa wanachunguza makaburi ya halaiki yaliyogundulika katika mgogoro kati ya vikosi vya usalama vya Congo na wapiganaji waasi wa kundi la Black Ant katika jimbo hilo la kati la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad