Msiba akumbushia amani kuelekea uchaguzi



Watanzania bila kujali itikadi za vyama, kabila na dini wote kwa pamoja wamekumbushwa kuilinda na kuitetea amani ya taifa kuelekea uchaguzi Mkuu utakaofanyika Mwezi Oktoba Mwaka huu ili kuendelea kuifanya Tanzania kubakia na amani ya kudumu. 

Ushauri huo umetolewa jijini Mwanza na Mwanaharakati huru, Cyprian Musiba wakati akizungumuza na waandishi wa habari kuelezea  mtazamo wake juu ya muenendo wa taifa kuelekea uchaguzi mkuu Mwaka huu. 

Musiba alisema iwapo kila mtanzania atatanguliza maslahi ya Taifa badala ya kuangalia zaidi maslahi ya vyama basi ni wazi kuwa Tanzania haiwezi kuingia kwenye machafuko daima na hata matukio yenye viashiria vya uvunjifu wa amani hayawezi kujitokeza kamwe. 

Alisema mchakato wa uchaguzi ni muhimu kwa  Taifa lolote lenye milengo ya kidemokrasia hivyo ni vyema kila mtanzania kwa nafasi yake ikiwemo vyombo vya habari kushiriki bila kusahau kuilinda amani kwa kuwa ndio kitu pekee chenye kutoa fursa ya kufikia malengo ya kitaifa yenye maslahi kwa kila mtu. 

Pia aliviomba vyama vya siasa kutokutumia majukwaa ya kisiasa kuwagawa watanzania bali navyo vihamasishe wanachama  wake kujiepusha na magenge yenye kuhatarisha demokrasia, uhuru na amani ya Taifa kwa kufanya hivyo kila chama kitakuwa kinaitakia mema nchi yetu. 

Aidha alitumia fursa hiyo kuishauri serikali kuhusiana na mchakato wa kuteua wabunge wa viti maalum ambao upo kikatiba ambapo alisema ni vyema viti maalumu vibakie kuwa kwa ajili ya walemavu pekee ili kuongeza uwakilishi wao kwa kuwa wao hawana uwezo wa kusimama kwenye majukwaa. 

Alisema imefika wakati sasa wanawake wabakie kuwezeshwa tu na siyo kuangaliwa kama kundi maalumu bali makundi maalumu yabakie kwa walemavu pekee na ndiyo wenye kustahili viti maalumu bungeni kwa kufanya hivyo taifa litakuwa limefanya kitu kikubwa chenye kuwaunganisha watu wote.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad