Nyota wa Muziki nchini Nigeria Davido amesema huu ni muda wa kubadilisha maisha yake na hataki mtu yoyote amtafute.
Sanjali na hilo, Davido amesisitiza kuuelewa ujumbe wake huo kwenye ukurasa wake wa Instagram, huku akiweka wazi kuwa atarudi baada ya kuachia Album yake mpya ya 'A Better Time'
Kauli hiyo ya Davido imekuja baada ya siku chache zilizopita Staa huyo kuripotiwa kuhama alipokuwa akiishi zamani na kuhamia Banana Island kwenye jumba lake la KIFAHARI.
Kuhusu Banana Island, hiki ni kisiwa kidogo kilicho tengenezwa huko Ikoyi Lagos nchini Nigeria, ni kama Paradise ya matajiri na ndio waliojaa huko na wanapapenda kwa sababu kuna amani, utulivu na vilevile ni mbali pia. Kisiwa hicho kinatajwa kuwa ndio chenye watu wengi zaidi nchini Nigeria.