Mufti Mkuu: Hakutokuwa na Ibada ya Hijja Mwaka Huu




Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir bin Ally kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), ametangaza kuwa mwaka huu hakutokuwa na ibada ya hijja hii ni kutokana na kauli iliyotolewa wiki hii na serikali ya Saudi Arabia kutokana na janga la Corona.

 

Abubakar Zubeir bin Ally ameyasema hayo leo Juni 25, 2020 wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa janga la Corona ndio limesababisha na haitakuwa kwa Tanzania pekee tu bali kwa Dunia nzima isipokuwa waislam waliopo ndani ya Saudi Arabia.

 

Ameeleza kuwa BAKWATA wameunga mkono maamuzi hayo ya Saudi Arabia lengo likiwa ni kuweka usalama kwa waumini na kuwakinga na Corona kwasababu ugonjwa huo ni wa kuambukiza.

 

Aidha, Mufti Zubeir amezitaka madrasa zote nchini kuanzia sasa kurejesha shughuli zote za madrasa nchini huku zikizingatia taratibu zote za kiafya kama inavyoshauriwa na wataalamu wa afya nchini.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndugu Mhariri, Kichwa cha Habari ni
    POTOSHI, Ni Lazima urudie kwa kuomba Usahihishaji hapa Hapa katika blogu yet

    kichwa kingeandikwa Hajj ya Mwaka huu
    ni kwa Waisilamu walioko ndani ya nchi
    ya Saudi Arabia, ingependeza na ndicho
    kilichopo. hajalishi Utaifa na Hajj ipo na ibada itafanyika, ila si mkusanyiko wa mahuja toka nje ya SAUDIA.

    TAFADHALINI TUWWE MAKINI NA VICHWA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Swadakta Mdau, Vichwa ndivyo Sivyo.

      "Abubakar Zubeir bin Ally ameyasema hayo leo Juni 25, 2020 wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa janga la Corona ndio limesababisha na haitakuwa kwa Tanzania pekee tu bali kwa Dunia nzima isipokuwa
      WAISLAM WALIOPO NDANI YA SAUDI ARABIA".

      KWA HIYO IBADA YA HIJJA IPO.. ILA WATOKA NCHI ZA NJE NDIO
      HAWATOFIKA KWA KULINDA NA KUOGOPA MAMBUKIZI YANAYOWEZA
      KUTOKEA.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad