Mwanafunzi Auawa Akiwa Kanisani Akijisomea




Wanigeria wamezua hamaki mitandaoni kufuatia mauaji ya kinyama ya mwanafunzi mwenye miaka 22, Uwavera Omozuwa aliyeuawa kanisani. Kampeni ya kutaka atendewe haki imeenea kwenye mitandao ya kijamii nchini Nigeria, huku familia yake ikiomba msaada wa kumtafuta muuaji.

Uwavera alikuwa anajisomea ndani ya kanisa la Redeemed Christian Church of God(RCCG) Kulingana na dada yake marehemu,Judith Omozuwa, Uwavera alikuwa anajisomea vitabu vyake ndani ya kanisa la Redeemed Christian Church of God(RCCG), karibu na nyumbani kwao Benin City .

Familia yake ilipokea simu kutoka kwa mama mmoja wa kanisa hilo mnamo Jumatano, Mei 27. Judith alifichua kwamba dada yake mpendwa alibakwa kabla ya kuawa na wahalifu hao. Uwavera alikua amejiunga na Chuo Kikuu cha Benin kusomea microbiolojia,Dada huyo alisimulia kwamba Uwavera alikimbizwa hospitalini baada ya mlinzi kupata sketi yake ikiwa imechanika na blauzi yake ikiwa imelowa damu.

Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa muuguzi, alikata roho hospitalini siku ya Jumamosi, Mei 30, kutokana na majeraha aliyopata baada ya kushambuliwa. Mwanzilishi wa kanisa la RCCG E.A. Adeboye ameshtumu tukio hilo na kutaka kila mmoja kuombea familia ya marehemu ili wapate haki.

#CHANZO BBCSWAHILI


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad