Mwenyekiti Wa Chadema Mkoa Wa Singida Atimkia CCM



Mjumbe wa Kamati Kuu na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Munde Tambwe (kulia) akimkabidhi kadi ya CCM, Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Singida, Shabani Limu baada ya kujiunga na chama hicho mwishoni mwa wiki

 

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Singida,.Shabani Limu amerejea Chama Cha Mapinduzi na kupokelewa kwa shangwe na nderemo..

Limu alipokelewa juzi na kukabidhi kadi ya Chadema kwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Munde Tambwe.

Akizungumza wakati wa hafla ya kumpokea mwanachama huyo mwishoni mwa wiki, Tambwe alimpongeza Limu kwa kurudi nyumbani kujakuongeza nguvu hasa katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.



“Karibu nyumbani tushirikiane kuendelea kukijenga chama chetu cha CCM chama cha wanyonge na kinacho pendwa ndani na nje ya nchi yetu alisema Tambwe.

Limu akizungumza baada ya kurejea CCM alisema ameridhishwa na mwenendo imara wa Chama Cha Mapinduzi katika kushughulika na changamoto za wananchi na yuko tayari kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika kuimarisha kazi anayoifanya Rais Dkt. John Magufuli ya kuwatumikia wanyonge.

” Rais wetu amefanya mambo makubwa katika nchi hii nimeona sina sababu ya kubaki Chadema bali nirudi CCM nyumbani kushirikiana na wanachama wenzangu kwa ajili ya kuchochea zaidi maendeleo ya Mkoa wa Singida” alisema Limu.

Limu alitumia nafasi hiyo kuwasihi wapinzani wengine wanaopenda maendeleo ya nchi yetu kuwa hawana sababu ya kuendelea kubaki huko waliko huku wakinyanyasika na kutengeneza maendeleo ya mtu pasipo maendeleo ya wananchi,,,warejee CCM kuijenga nchi na kuwa sasa Singida imeshaseti mitambo na iko tayari kuingia kwenye uchaguzi.

Na Dotto Mwaibale, Singida


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad