Nilikuwa Mateka wa Pombe- Vanessa Mdee Asimulia Shimo Kubwa Alimojiondoa


Vanessa Mdee  amekuwa akifichua  mengi kuhusu maisha yake  ya  miaka ya hapo nyuma kupitia podcast yake  , Deep Dive with Vanessa Mdee.  Nyota huyo  maajuzi ameacha muziki ili kufanya mambo mengine.


Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 32  ametoa ufichuzi wa jinsi unywaji pombe nusra uvuruge maisha yake na kumfanya kutoa maamuzi ambayo mengi anajutia . amesema wakati mmoja alikuwa akiishi kama roboti  na kwamba hakuwa hata akijitambua  nayo mawazo yakamzonga fikra .

“ Nilianza kuwa mtu wa kufanya maamuzi  mabaya   na hata sikuweza kujitambua’

“ Nyakati nyingi nilijipata katika hali za mawazo kupindukia na sikujua cha kufanya  ,Presha hiyo ilikuwa ya juu zaidi kwa mtu yeyote  ,na kipi kinachofuatia?’


Anasema kama mraibu wa utumizi wa dawa za kulevya alijipata akiwa stadi sana wa kuficha vitu vingi vilivyokuwa vikimfanyikia maishani .

“ Nilifanya mambo mengi vizuri  na hakuna aliyejua nilikuwa nazongwa na mawazo wala kutekwa nyara na utumizi wa pombe’


Ufichuzi huo wake unajiri baada ya nyota huyo kutangaza kwamba amejiondoa katika fani ya muziki alioitaja kama ya kishetani .  Mdee hata hivyo sasa  ana mtu wa kumpa bega  baada ya kujitosa mapenzini na  muigizaji wa kipidi cha Power  Rotimi .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad