Nimeisambaratisha CHADEMA Ukonga, sasa nahamia Tarime Vijijini- Mwita Waitara


Naibu Waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara, amesema kuwa mpaka sasa hivi amekwishamaliza kazi kubwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam ya kukisambaratisha Chama cha CHADEMA, na kwa sasa  ameweka wazi kwa mara nyingine kuwa atakwenda kugombea ubunge katika jimbo la Tarime Vijijini mkoani Mara kupitia chama hicho.

Waitara amesisitiza kuwa haondoki Ukonga kwa sababu anamkimbia mtu, bali amekamilisha kazi ya kukisambaratisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hivyo anakwenda Tarime Vijijini ambako ndipo anapotokea, kufanya kazi hiyo.

“Wala hakuna mtu ninayemkimbia, jimbo langu [Ukonga] lipo salama ndani na nje ya chama. Nimeshafanya kazi ya kuwasambaratisha CHADEMA hapa wameshapoteana. Walikuwa na Meya wa Jiji, hayupo, walikuwa na Meya Ilala, hayupo, walikuwa na Meya wa Ubungo, hayupo. Nishamaliza kazi Dar es Salaam, naenda kukamilisha kazi sehemu nyingine,” amesema Waitara.

Kiongozi huyo ambaye alihamia CCM akitokea CHADEMA Julai 2018 amesema kuwa Julai 14 mwaka huu atachukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Tarime Vijijini, na kwamba suala hilo sio siri
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yes Mwita. Ndiyo inavyo taka na kutakiwa.. Uruguay mtindo mmoja kwa Hawa VIBARAKA.. Tuendelee kucheza nao.. MPAKA kigenga Cha mwisho.. Liwe Jua iwe MVUA TARIME vijijini tunakujaHeche enda SENGEREMA Boys. AJIRA zipo ila kumbuka Vigezo na Mashariti kuzingatiwa. Tutahakiki vyeti vyako mwanzo na kama FEKI hatua stahiki itachukuliwa. Karibu SENGEREMA bro.

    ReplyDelete
  2. Yes Mwita. Ndiyo inavyo taka na kutakiwa.. Uruguay mtindo mmoja kwa Hawa VIBARAKA.. Tuendelee kucheza nao.. MPAKA kipenga Cha mwisho.. Liwe Jua iwe MVUA TARIME vijijini tunakuja Heche nenda SENGEREMA Boys. AJIRA zipo ila kumbuka: Vigezo na Mashariti kuzingatiwa.

    Tutahakiki vyeti vyako mwanzo na kama FEKI hatua stahiki zitachukuliwa.

    Karibu SENGEREMA bro. Kijani Oyee
    Umemsikia Ester kakwambia je?
    Amka Bro, AJIRA isikupite.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad